Serikali
ya Tanzania, imezipa msisitizo wizara mbalimbali kuhakikisha zinahamishia makazi yake Makao
Makuu ya nchi mkoani Dodoma kabla ya Februari 28, mwaka huu,2017 kama
ilivyotangazwa na Rais John Magufuli mwaka jana 2016.
Akizungumza na Waandishi wa habari January 19,2017, Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu, Sera, Bunge,
Kazi, Ajira, Vijana na Ulemavu, Mhe.Jenista Mhagama, alisema agizo la serikali
lazima liwe limetekelezwa ifikapo Februari 28, mwaka huu.
“Kama agizo
lilivyotolewa na Rais Magufuli kuhusu wizara na watumishi wake kuhamia Makao
Makuu Dodoma, ndivyo wanavyotakiwa Manaibu Makatibu Wakuu, Makatibu, Manaibu
Mawaziri na Mawaziri kutakiwa kuwapo Dodoma mwishoni mwa Februari,” alisema
Mhagama.
Waziri
Mhagama alisema ofisi yake imeweza kukagua miundombinu na ujenzi wa majengo
mbalimbali ya serikali yanayoendelea kujengwa na mengine yakiwa yamekamilika
kwa ajili ya matumizi ya wizara hizo.
“Hakuna
tatizo la ofisi za watumishi wa wizara zote, kwani majengo yamekamilika na yapo
katika hali nzuri tayari kwa ajili ya kuanza kutumiwa, hivyo wakuu husika
wakiwamo mawaziri wahakikishe wanatakiwa kuhamia Dodoma,” alisema.
|
No comments:
Post a Comment