VIDEO: Penati 4-2 Yanga SC ikitolewa...Sasa ni Simba SC vs Azam FC fainali Mapinduzi Cup 2017. - Mwana Wa Makonda

Muhtasari

X-BET


Post Top Ad

Wednesday, January 11, 2017

VIDEO: Penati 4-2 Yanga SC ikitolewa...Sasa ni Simba SC vs Azam FC fainali Mapinduzi Cup 2017.

Yanga SC imeendelea kusulubiwa kwenye mashindano ya Mapinduzi Cup 2017 baada ya kujikuta ikichezea kichapo kutoka kwa Simba SC kwenye mchezo wa nusu fainali ya pili ya mashindano hayo Jana January 10, 2017 kwa mikwaju ya penati 4-2 kufatia dakika 90 kumalizika bila timu hizo kufungana kwenye Uwanja wa Amaan, Zanzibar.

Golikipa wa Simba SC, Daniel Agyei ndio alikuwa shujaa kwa upande wa Simba SC wakati wa changamoto ya mikwaju ya penati.  

Agyei ameokoa penati mbili za Deogratius Munishi na Mwinyi Haji huku yeye akifunga penati yake baada ya Jonas Mkude kufunga ya kwanza.

Simba SC sasa itakutana na Azam FC Ijumaa January 13, 2017 katika Fainali. Azam FC imeitoa Taifa Jang’ombe katika mchezo uliotangulia kwa bao 1-0.

HAPA CHINI BOFYA KUTAZAMA PENATI ZA SIMBA NA YANGA MAPINDUZI CUP  4-2

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad