Rais Dkt.
John Pombe Magufuli akiwapungia mkono wakazi wa Bariadi Leo hii January 11,2017, mara baada ya kumaliza
kufungua barabara ya Bariadi-Lamadi yenye urefu wa kilometa 71.8.
|
Rais Dkt.
John Pombe Magufuli akiweka jiwe la ufunguzi wa barabara ya Bariadi-Lamadi
yenye kilometa 71.8 .
Wengine katika picha ni
Mkuu wa Mkoa wa Simiyu Antony Mtaka, Naibu Waziri Ofisi ya Makamu wa
Rais Mazingira na Muungano Luhaga Mpina, Waziri wa Ujenzi Uchukuzi na
Mawasiliano, Profesa Makame Mbarawa, Mwenyekiti wa CCM Simiyu Titus Kamani na
Mbunge wa Bariadi Andrew Chenge.
|
Rais Dkt.
John Pombe Magufuli akikata utepe na
Mkuu wa Mkoa wa Simiyu Antony Mtaka pamoja na Waziri wa Ujenzi Profesa Makame
Mbarawa kuashiria ufunguzi wa barabara ya Barabara ya Bariadi-Lamadi yenye
kilometa 71.8.
|
Rais John
Pombe Magufuli, leo Januri 11, 2017 amefanya ziara na katika Wilaya ya Bariadi
mkoani Simiyu na kufanikiwa kuzungumza na mamia ya wananchi wa wilaya hiyo
katika waliojitokeza katika uwanja wa Shule ya Msingi Somanda wilayani humo.
Nimekuwekea
sentensi chache ikiwa ni sehemu ya hotubaya Rais Magufuli, Bariadi leo.
“Wanaolalamika
fedha hakuna ni wale waliokuwa wanafaidi fedha ambazo tumezichukuwa na
kuzipeleka kwenye maendeleo ya wananchi.
“Mimi
ninaopambana nao ni wale waliosababisha tukawa masikini, hao ndio nakula nao
sahani moja na naomba mniunge mkono.
“Tunataka
kuanzia mwaka kesho hapa Bariadi tujenge uwanja wa ndege. Wageni wakija hapa na
uchumi wa Bariadi utakuwa na tutanufaika mno.
“Katika
maendeleo machungu lazima yawepo. Ukitaka kufanya kazi lazima wawepo
watakaoumia.
Wakazi wa
mkoa wa Simiyu, nawaomba barabara hii muitunze ili iwatunze. Barabara hii nzuri
isiwe chanzo cha mauaji ya Watanzania.
“Lakini
muitumie barabara hii kwa ajili ya biashara, safirisheni bidhaa mbalimbali
ikiwemo mazao hata Dar es Salamm mkauzie huko.
“Naomba
msing’oe alama za barabara, hasa madereva wa baiskeli huwa mnangoa ‘reflector’
na kufunga kwenye baiskeli.”
“Mimi ni
mgumu sana kumpongeza mtu, lakini nakupongeza Mkuu wa Mkoa wa Simiyu, viongozi
wengine waige kutoka kwako. Mkuu wa Mkoa wa Simiyu ameanzisha programu wa
Wilaya Moja, Bidhaa Moja ambapo kila wilaya itakuwa ikizalisha bidhaa yake
tofauti na nyingine.
“Tumekuwa
tukitegemea mvua sana, lakini ni wakati wa kulima mazao ya muda mfupi na ambayo
hayahitaji maji mengi sana.
“Kuna watu
bado mzee bure hajatoka kichwani mwao kila kitu wanategemea serikali, serikali
yangu haitatoa kila kitu.
“Kuna
wengine Busega wamelima pembeni ya ziwa, mahindi yamekauka, yani ameshindwa
hata kumwagilia, nimesema sileti chakula. Wengine wanatumia magazeti kutangaza
kuna njaa ili walete mahindi kutoka Brazil wasamehewe kodi.
“Kuna mmoja
kaleta mahindi tani 25,000 kutoka Brazil hayana ubora na anataka asamehewe
kodi, nimesema tutakata kodi yote. Wabunge waliruhusu chakula kipelekwe Uganda
lakini wao leo ndio wanalia njaa, nimesema chakula sileti, fanyeni kazi.
“Nimeweka
jiwe la msingi kwenye hospitali leo hapa Simiyu nikaambiwa itatumia bilioni 46,
nasema haliwezekani chini ya uongozi wangu. Mimi nitaleta TZS bilioni 10 na
nataka jengo hilo la hospitali likamilike kwa hiyo fedha na si bilioni 46
mnazoniambia. Na jengo hilo likikamilika nitakuja kulizindua mimi.
Na kama kuna
kiongozi wa TBA anaweka cha juu, Waziri Mbarawa mfukuze kazi.
“Wananchi
mmezoea sana kubembelezwa na kuambiwa maneno mazuri, ni wakati sasa niwaambie
ukweli hata kama unauma. Jiwe nitaliita jiwe, sitaliita mchanga uliokusanyika
pamoja.
“Nataka
hospitali hii ikamilike kwa gharama ambazo hata ukimwambia mtoto mdogo
atakuelewa na si kukushangaa. Wakala wa Barabara Tanzania (TanRoads) ni watatu
kwa ubora Afrika, ya kwanza ni ya Afrika Kusini, Namibia alafu Tanzania.
Mkataba wa hii barabara unataka mhandisi akishakabidhi barabara, likitokea
shimo kwa miaka miwili ajaziba kwa gharama zake.
“Tumenunua
ndege 6, tutanunua meli kuwa Ziwa Victoria, tunajenga reli ya kisasa ya kati,
lakini wapinzani hawayaoni haya mazuri. Serikali inafanya mambo mengine
makubwa. Sasa msitegemee serikali ifanye haya yote na chakula iwagawie,
haiwezekani.
Mbali na
hayo, Rais Magufuli amemhoji Mhandisi wa maji Busega kumtaka aseme ni lini maji
yatafika mjini hapo huku akiagiza kufutwa kwa leseni ya mwekezaji wa madini
Bariadi endapo ataona kuwekwa tenki la maji kutamzuia kuchimba madini.
“Maji ni
yetu na madini ni yetu, haiwezekani watanzania hawa wakose maji kwasababu eti,
mwekezaji atashindwa kuchimba madini. Tena ikiwezekana mwambieni huyo mwekezaji
hilo tenki atujengee yeye. Tenki lijengwe juu yeye madini ayachimbe chini.
“Mimi si
Rais, urais ni wenu ninyi mliosimama kwenye jua na mvua tena mkiwa na njaa
mkapiga kura, sina cha kuwalipa. Inawezekana nisiwe mwanasiasa mzuri lakini
siku moja mtakumbuka niliyoyafanya. Nia yangu ni nzuri mbele yenu ya mbele ya
Mungu.” Alisema Rais Magufuli.
Rais
Dkt Magufuli akamaliza kuzungumza na
wananchi wa Bariadi kwa kuwataka kuiunga mkono serikali yake katika kupambana
na rushwa pamoja na ufisadi sambamba na kuwasihi kufanya kazi kwa bidii kwa
ajiliya maendeleo yao na taifa kwa ujumla.
|
No comments:
Post a Comment