Waziri Mkuu
Mstaafu na Mgombea wa Urais 2015 kupitia CHADEMA, Bw.Edward Lowassa Jana
January 16,2017 alikamatwa na jeshi la
Polisi wakati akiwa anaenda kwenye
kampeni za uchaguzi Kata ya Nkome na baadaye aliachiwa huru ambapo taarifa za polisi zinadai kuwa
walimzuia kwa sababu za kiusalama.
Mbali na hivyo, Polisi walilazimika kutumia
mabomu ya machozi kuwatawanya wananchi walioandamana kwenda kituo cha polisi
baada ya Lowassa kukamatwa.
Aidha
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Geita,ACP Lotson Mponjoli, amesema kuwa hawakuwa
wamemkamata Edward Lowassa bali walikuwa wakijadiliana naye kuhusu usalama wake
na jamii.
|
Kupitia
kituo cha Television cha Azam wameripoti habari ya kukamtwa kwa Lowassa ambapo
baadhi wa wananchi wameeleza ilivyokuwa.
"Tulikuwa
kwenye msafara ya kumpokea Lowassa lakini tulipofika hapa stendi wananchi
walitaka kuongea na Lowassa, kabla hata hajashuka kwenye gari askari
walituvamia wakasema tuondoke moja kwa moja twende kituoni"- shuhuda
''Sikiliza
mkasa mzima hapo chini
|
No comments:
Post a Comment