Kagera Sugar imeifunga Ndanda FC 2-0 -Ligi Kuu Tanzania bara 2-16/2017. - Mwana Wa Makonda

Muhtasari

X-BET


Post Top Ad

Saturday, January 14, 2017

Kagera Sugar imeifunga Ndanda FC 2-0 -Ligi Kuu Tanzania bara 2-16/2017.

Ligi Kuu Vodacom, ilikuwepo Leo January 14,2017 kwenye Viwanja Viwili na kushuhudia Timu za Nyumbani zote zikishinda 2-0.

 Huko Shinyanga, Stand United imewacharaza wenzao wa Mkoa huo Mwadui FC Bao 2-0 kwa Bao za Jacob Massawe na Adeyum Salehe na kujikita Nafasi ya 6 wakati Mwadui wapo wa 10.

Huko Kaitaba Mjini Bukoba, Kagera Sugar imeifunga Ndanda FC 2-0 kwa Mabao ya Mbaraka Yusuph aliefunga zote.

Ushindi huu umewaweka Kagera Sugar Nafasi ya 3 wakati Ndanda FC wakiwa wa 13.

VPL itaendelea Jumapili kwa Mechi 1 huko CCM Kirumba, Mwanza kati ya Mbao FC na African Lyon.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad