AFCON 2017 -DR Congo yaitwanga Morocco 1-0. - Mwana Wa Makonda

Muhtasari

X-BET


Post Top Ad

Tuesday, January 17, 2017

AFCON 2017 -DR Congo yaitwanga Morocco 1-0.

Jamhuri ya Kidemokrasi ya Kongo ,DRC imeweka matatizo yake ya malipo pembeni na kuicharaza Morocco kwa 1-0 kwenye mchezo wake wa ufunguzi wa Kombe la Mataifa ya Afrika nchini Gabon-AFCON 2017 mchezo uliochezwa Jana January 16,2017 kwenye uwanja wa Stade d'Oyem.

Ushindi huo umepatikana kupitia bao la Junior Kabananga aliyefunga katika dakika ya 55 ya mchezo huo.

DRC walimaliza wakiwa mchezaji mmoja pungufu baada ya Lomalisa Mutambala kutolewa nje kwa kuoneshwa kadi mbili za manjano. Mutambala aliingia kama mchezaji wa akiba, na kutolewa baada ya dakika 16.
DRC walilazimika kucheza wakiwa tisa tu uwanjani kwa muda baada ya Mutambala kutolewa na beki Gabriel Zakuani kuumia na kutoka nje.

Kwa ushindi huo, DR Congo sasa inaongoza Kundi C kwa alama 3 baada ya mchezo wa awali kati ya Mabingwa watetezi Ivory Coast kutoka sare ya 0-0 na Togo.

Leo  Jumanne,January 17,2017 zipo Mechi mbili za Kundi D kati ya Ghana na Uganda na kisha ni

Mali na Egypt zote zikichezwa Oyem Stadium, Mjini Assok Ngomo huko Gabon.

AFCON 2017

Ratiba/Matokeo:

**Saa za Bongo

Mechi za Makundi

Jumamosi Januari 14,2017

Kundi A

Gabon 1 – 1 Guinea-Bissau

Burkina Faso 1 – 1 Cameroon

Jumapili Januari 15,2017

Kundi B

Algeria 2 – 2 Zimbabwe

Tunisia 0 – 2 Senegal

Jumatatu Januari 16,2017

Kundi C

Ivory Coast 0 – 0 Togo

 Congo DR 1 – 0  Morocco

Jumanne Januari 17

Kundi D

1900 Ghana v Uganda

2200 Mali v Egypt

Jumatano Januari 18,2017

Kundi A

1900 Gabon v Burkina Faso

2200 Cameroon v Guinea-Bissau

Alhamisi Januari 19,2017.

Kundi B

1900 Algeria v Tunisia

2200 Senegal v Zimbabwe

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad