Kamishna
Msaidizi wa Ustawi wa Jamii Bi Beatrice Fungamo kutoka Wizara ya Afya,
Maendeleo ya Jamii, Jinsia Wazee na Watoto akikabidhi kwa niaba ya Rais zawadi
ya Sikukuu kwa Msimamizi wa Kituo cha Watoto Mburahati jijini Dare es Salaam.
Na Anthony
Ishengoma
Rais John
Pombe Magufuli ametoa zawadi yenye thamani ya shilingi 8,475,000 kwa watu walio katika makundi maalum wakiwemo
watoto walio katika mazingira hatarishi na wazee wanaohudumiwa katika makazi
ili waweze kusherehekea sikuu ya krismass ya mwaka 2016 na mwaka mpya 2017.
Akikadidhi
zawadi hizi kwa niaba yake Kamishna Msaidizi wa Ustawi wa Jamii Bi
Beatrice Fungamo kutoka Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia Wazee na
Watoto amesema ni utaratibu wa kawaida kwa viongozi Wakuu wa Nchi yetu kuwapatia
makundi haya maalum zawadi ya Siku Kuu Krismass ya mwaka huu na mwaka mpya.
Zawadi
zilizotolewa kwa thamani hiyo ya fedha ni vyakula kama vile mchele, mbuzi na
mafuta ya kupikia ili kuwawezesha kufurahi na kusherehekea sikukuu kama ilivyo
kwa watu wengine.
Zawadi hizi
zimetolewa kwa vituo 7 katika Mkoa wa Dar es Salaam, vituo viwili kutoka
Zanzibar na Makazi ya Wazee katika mikoa ya Tabora, Kilimanjaro, Manyara,
Kigoma, Tanga, Ruvuma, Shinyanga, Singida, Mwanza, Lindi, Mtwara, Kagera, Mara
na Morogoro.
Bi. Beatrice
Fungamo amevitaja vituo hivyo kutoka mkoa wa Dar es Salaam kuwa ni Makao ya
Taifa ya Watoto Yatima Kurasini – Temeke, Makao ya Watoto Msimbazi, Kituo cha
Watoto Dar Al Arqum, Makao ya Watoto Mburahati, Makao ya Watoto Kijiji cha
Furaha, Mahabusu ya Watoto Dar es Salaam, Upanga na Makazi ya Wazee Wasiojiweza
na wenye Ulemavu Nunge, Kigamboni.
Aidha kutoka
Zanzibar ni Kituo cha Watoto Mabaoni - Chakechake, Pemba na Makazi ya wazee
wasiojiweza Sebleni – Unguja ikiwemo makambi ya wazee kutoka mikoa yote ya
Tanzania Bara yenye makambi ya Wazee.
|
Post Top Ad
Saturday, December 24, 2016

Rais Magufuli Atoa zawadi ya Sikukuu kwa Watu walio katika Makundi Maalum.
Tags
# MATUKIO
Sambaza Hii
Chief Editor | Mhariri
Journalist / Chief Editor / Tanzanian Blogger
Simu: 0756830214 / 0620197747 / 0789925630.
Makala Inayofuata
Watanzania tuchape kazi kwelikweli kwa sababu hakuna cha bure – Rais Magufuli.
Makala Iliyopita
Kingunge Asema Bila tume huru Wapinzani Wasahau Kuingia Ikulu .......Lowassa Akubali Yaliyopita Si Ndwele.
Muonekano wa Uwanja wa CCM Kirumba Jijini Mwanza.
AnonymousDec 10, 2019Viongozi Wilayani Kasulu watakiwa Kuimarisha Usalama Katika Korongo la Bolelo.
AnonymousJun 29, 2019Shirika la Ndege la Tanzania Laanza Safari za Afrika Kusini Leo 28/06/2019.
AnonymousJun 28, 2019
Labels:
MATUKIO
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment