Aidha kwa mahitaji ya haraka tayari
Kamati ya mkoa imegawa chakula kwa wahanga katika mkoa mzima kama ifuatavyo:
unga wa sembe kilo 3750, mchele kilo 1850, sukari tani 6.5, maharage kilo 3470,
bisukuti katoni 2600, na maji ya kunywa katoni 615.
Pia wahanga wamegawiwa
mahitaji muhimu kama mablanketi 480 mahema 119 na matrubali 320.
Huo ulikuwa
ugawaji wa mahitaji wa awali na kamati zinaendelea kugawa mahitaji hayo katika
maeneo yaliyoathirika na yataendelea kugawiwa kadri tunavyopokea misaada ya
mahitaji hayo.
Napenda sasa kutoa taarifa ya
michango mbalimbali ambayo tayari tumeipokea kutoka kwa wadau mbalimbali;
Katika Harambee tuliyoifanya tarehe 16/09/2016 tuliweza kukusanya kiasi
cha fedha taslimu pamoja na hundi 7,800,000/=, ahadi ya fedha na vifaa ni
shilingi milioni 770,502,000/= kama wadau hawa wote watatoa michango yao jumla
tutakuwa tumepata shilingi milioni 778,302,000/=
Kupitia Akaunti yetu iliyoko Benki ya CRDB inayojulikana kama “KAMATI YA
MAAFA KAGERA CRDB BUKOBA” Akaunti Namba 0152225617300 tayari tumekusanya kiasi
cha shilingi 623, 624,200/=.
Aidha, baada ya Mhe, Waziri Mkuu kuzindua namba za
simu za kuchangia maafa Kagera tayari wananchi wameanza kuchangia michango yao
kupitia namba hizo ambazo ni (M.PESA 0768 196 669), (AIRTEL MONEY 0682 950
009), (TIGO PESA 0718 069 616).
|
No comments:
Post a Comment