|
Mamlaka ya
Vitambulisho vya Taifa (NIDA) imeeleza kuwa ifikapo Desemba 31 mwaka huu jumla
ya watanzania milioni 23 watakuwa na namba za utambulisho wa vitambulisho vya
Uraia.
Kaimu Mkuu
wa Kitengo cha Mawasiliano wa Mamlaka hiyo Bi. Rose Mdami amesema kuwa hatua
hiyo ni utekelezaji wa agizo Rais, Dkt. John Pombe Magufuli la kuitaka Mamlaka
hiyo kuweka saini ya mwombaji na mtoaji wa vitambulisho hivyo.
“Tumeanza
kutekeleza agizo la Mhe. Rais tangu mwezi Juni mwaka huu, hii inamaanisha
kwamba vitambulisho vyote tulivyochapisha kuanzia mwezi Juni mpaka leo vina
saini ya muombaji, saini ya mtoaji na tarehe ya kuzaliwa muombaji” amefafanua
Mdami.
Ameeleza
kuwa kazi ya ugawaji wa vitambulisho hivyo inasubiri kuzinduliwa na Mhe. Rais
Dkt. John Pombe Magufuli atakayekabidhiwa
kitambulisho cha uraia namba moja na baadaye vitambulisho hivyo kugawiwa
kwa wananchi wengine.
Mdami
amesema ifikapo Desemba 31 mwaka huu NIDA itakuwa imetoa namba za utambulisho
wa vitambulisho hivyo kwa watanzania
milioni 23 kwa kutumia taarifa za Tume ya Uchaguzi (NEC) zilizo katika
vitambulisho vya kupigia kura na kuziamishia katika kanzi data ya NIDA.
Amefafanua kuwa ili mwananchi aweze kupata kitambulisho
cha uraia atalazimika kufika katika ofisi za NIDA akiwa na vielelezo
vinavyoonyesha mwaka wake wa kuzaliwa pamoja uthibitisho wa uraia wake hii ni
kutokana na NEC kutokuwa na viambatanisho hivyo.
Amebainisha
kuwa mwananchi mwenye namba ya utambulisho anaweza kupata huduma zote
zinazohitaji namba ya kitambulisho cha Uraia kutokana na namba hiyo
kutobadirika na kuendelea kutumika hata baada ya kitambulisho kuchapishwa.
Amesema
mpaka sasa watanzania milioni 2.7 wamekwisha patiwa vitambulisho hivyo na milioni 6.5 wamesajiriwa kwa ajili
ya kupata vitambulisho hivyo.
Aidha,
Vitambulisho hivyo vya zamani vitaendelea kutumika mpaka utakapotangazwa
utaratibu wa kuvibadirisha kwa ajili ya kupata vitambulisho vipya.
Pia ametoa
ufafanuzi juu ya malalamiko ya baadhi ya watu wanaodai kwamba wa kumekuwa na
mlolongo mrefu wa kupata vitambulisho hivyo kwa kueleza kuwa NIDA haina namna
ya kufupisha mlolongo huo kwani kufanya hivyo ni sawa na kuuza uraia wa
Tanzania.
Amesisitiza kuwa ni lazima NIDA ijiridhishe
juu ya uhalali na sifa za muombaji ni kuwa ni Mtanzania kwa kuambatanisha
vielelezo vinavyohitajika.
|
No comments:
Post a Comment