|
Mwenyekiti
wa chama cha mpira wa Miguu Mkoa wa Kagera Jamal Emil Malinzi ambaye
amechaguliwa tena kikiongoza Chama hicho kwa mara nyingine kwa Miaka 4.
Akiongea na
Mtandao huu wa Bukobasports amesema kwa sasa wameanza na mkakati wa kuboresha
Uwanja wa Kaitaba kwa kuuwekea Nyasi bandia na kuongeza idadi ya Majukwaa ili
uweze kutumika kwa Michezo ya Kimataifa.
Pia Chama cha mpira wa miguu Mkoa
kimeomba Viwanja kwa ajili ya kujenga kituo cha michezo na Uwanja wa kwa
Ufadili wa FIFA jambo ambalo kimsingi linawezekana kila Mtu akitimiza wajibu
wake.
Pamoja na
hayo aliomba kupitia mkutano huo kuviomba Vyama vyote vya Wilaya kuomba maeneo
ya kujenga Viwanja vya mpira wa miguu kwenye Halmashauri zao husika.
Mwisho
aliwashukuru wote kwa nafasi zao na kuwaomba ushirikiano wa hali na mali ili
Mkoa wa Kagera uweze kuongeza Timu zingine
katika Ligi kuu Vodacom na Madaraja mengine.
|
|
Mjumbe
akitoa neno wakati wa Mkutano mkuu wa KRFA 2016 tarehe 14/08/2016.
|
|
Kwa Makini
sana wakimsikiliza Mjumbe
|
|
Malick Sudi
Tibabimale(kushoto) akisikiliza neno kwa makini kutoka kwa Mjumbe.
|
|
Mwenyekiti
wa chama cha mpira wa Miguu Mkoa wa Kagera Jamal Emil Malinzi ambaye
amechaguliwa tena kikiongoza Chama hicho kwa mara nyingine kwa Miaka 4
akipongezwa na Baadhi ya Wajumbe na Viongozi mbalimbali kwenye Ukumbi huo wa
Optima mara baada ya kushinda.
|
| Add caption |
|
Kushoto ni
Al-amin Abdul Abdul Kiongozi mpyaa wa chama cha Mpira Mkoa wa Kagera KRFA
ambaye amechaguliwa kuwa Katibu Msaidi ambapo Katibu ni Ndugu Saloum H. Umande
Chama. Al-amin Abdul amembwaga Ndg. Malick Sudi Tibabimale.
|
|
Viongozi
(Kamati Tendaji) waliochaguliwa leo kukiongoza Chama cha Soka Kagera KRFA.
|





No comments:
Post a Comment