Serikali yaombwa Kuboreshea miundo mbinu ya Maji katika Vijiji Nyagwijima, Mugunzu na Kakonko. - Mwana Wa Makonda

Muhtasari

X-BET


Post Top Ad

Monday, August 15, 2016

Serikali yaombwa Kuboreshea miundo mbinu ya Maji katika Vijiji Nyagwijima, Mugunzu na Kakonko.


Wakazi wa Vijiji Nyagwijima, Mugunzu na Kakonko wilaya  Kakonko Mkoani Kigoma wameiomba serikali kuwaboreshea miundo mbinu ya maji ili waweze kuondokana na Tatizo la uhaba wa maji kwenye vijiji vyao kwa kutembea mwendo mrefu wakitafuta bidhaa hiyo hatua inayowakwamisha katika shughuli zao za uzalishaji mali.

Wakiongea na Waandishi wa Habari kwa nyakati tofauti  baadhi ya wananchi  ambao ni Rosemary Rafael na Secelie Ntungie wamesema  katika maeneo mengi ya vijijini ambako ndiko  nguvu kazi kubwa ya uzalishaji mali iliko, kuna shida kubwa ya maji nakueleza kuwa magati  mengi ya kutolea maji  yamesimikwa tu bila kutoa maji na kulazimika kuyafuata umbali mrefu.

‘’ Serikali imekuwa ikielekeza nguvu nyingi kwa huduma mbalimbali ikiwemo maji katika maeneo ya Mijini tofauti na vijijini hatua inayopelekea shughuli za uzalishaji mali kutokuwa na mafanikio mazuri kwa kuwa wananchi wengi hasa majira ya kiangazi maeneo mengi ukauka na kuwalazimu kutumia muda mwingi wakitafuta maji alisemaalisema Rosemary’’

Pamoja na wananchi kuhangaika kutafuta maji, upo mradi wa maji  unaofadhiliwa na Benk ya Dunia katika vijiji ambapo kama taratibu zingewekwa vizuri, uenda  unafuu ungepatikana kwa wananchi, ambapo Madiwani katika kikao cha Baraza hilo kwa ajili ya kujadili mswala ya maendeleo ya wananchi  wamesema kutokana na wilaya ya kibondo kutokabidhi miradi ya maji kwa wilaya ya Kakonko kumesababisha usumbu wa kukosa maji,  kwa sababu hapo awali kabla ya wilaya kugawanywa iliku ikisimamiwa na wailaya ya kibondo hadi sasa.

Akitoa kauli hiyo kwenye baraza hilo juzi Diwani Viti maalum Tarafa ya Nyaronga Fides Mahagara, alisema miradi ya maji iliyolenga vijiji kumi, vitano kakonko na vitano Kibondo haijakabidhiwa kwa wananchi ili iweze kuanza kufanya kazi ambapo wananchi wanaambulia kuona mabomba yasiyotoa maji.
 
Kikao hicho cha Baraza la Madiwani, kilimtaka Mwandisi wa maji toka Kibondo, Michael Nguruwe kutoa maelezo kwanini miradi ya maji upande wa kakonko inaenedelea kumilikiwa na wilaya ya kibondo, alisema kwa mujibu wa wizara, inatakiwa mafunzo yatolewe kwa kamati za maji vijijini wafahamu taratibu za uendeshaji miradi ikiwemo mitambo ya kusukuma maji na kusema fedha  ziko katika halmashauri ya kakonko.

Mkuu wa wilaya hiyo,Kanali Hosea Ndagala -(Pichani) 

 Nae mwandisi wa maji Halmashauri ya Kakonko Herinathani Elisha alipoulizwa na mwenyekiti wa Halmashaa, sababu gani inazuia utaratibu uliopangwa usifanyike, na atoe maelezo miradi hiyo itakabidhiwa lini, licha ya madai kuwa imekamilika kwa asilimi 98 huku hata maji katika maeneo mengi hayatoki, alisema ataazanza kutoa mafunzo ndani ya wiki mbili kuanzia sasa na bidhiwa wahusika.

Hata hivyo Mwenyekiti wa halmashauri ya wilaya ya Kakonko Juma Maganga, aliliomba Baraza hilo kutoa muda wa mwezi mmoja mwandisi huyo awe amekabidhi miradi hiyo na kueleza kuwa vitendo vya kutokujali vimekuwa vikiwakasirisha wahisani na kuwafanya waanze na  kutoa fedha  zao wakihofia ubadhilifu.
 
 Kabla ya wilaya ya Kibondo kugawanywa na kuwepo wilaya mpya ya Kakonko, mambo mengi yalisimamiwa halmashauri ya Kibondo na hata baada ya kuzaliwa wilaya Kakonko Miradi ya Maji inayofadhiliwa na Benk ya Dunia iliendelea kuwa chini ya halmashauri ya Kibondo..HABARI/PICHA NA MUHINGO MWEMEZI-KIBONDO

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad