|
Mgari ya
kubeba wagonjwa yaliyotolewa na shirika la umoja wa mataifa Unicef kwa ajili ya
halmashauri ya kakonko.
Halmashauri
ya wilaya ya Kakonko mkoani Kigoma imepokea Magari mawili ya kubeba wagonjwa
aina ya Toyota Land Cruiser yaliyotolewa na shirika la umoja wa mataifa la
kuhudumia Watoto Unicef ambapo magari hayo yanalenga kupunguza adha na kuokoa
maisha ya wanawake wajawazito na watoto.
Katika hafla
ya makabidhiano ya magari hayo,
iliyofanyika jana mjini Kakonko, Mkurugenzi mtendaji wa Halmashauri hiyo, Bw.
Lusubilo Joel, alisema kuwa kutokana na adha wanazozipata wanawake wajawazito
na watoto, shirika hilo la UNICEF limetoa magari hayo kwa mkopo ambao utalipwa
kwa muda wa miaka mitano na kuitaka idara ya afya ya wilaya hiyo kuyatumia kwa
malengo mahususi ili yaweze kuleta tija.
Mkuu wa wilaya hiyo,Kanali Hosea Ndagala -(Pichani) alipokuwa
akikadidhi magari hayo kwa Mganga mkuu wa wilaya, ambapo moja litatumika katika Kituo cha afya
Kakonko ambacho kinatumika kama Hospital ya wilaya, na lingine litapelekwa
katika kituo cha Nyanzige Tarafa ya nyaronga amesema kuwa ni vema utunzaji wa
mali za umma ukatiliwa mkazo ili kuepuka hasara zisizokuwa za lazima.
|
No comments:
Post a Comment