|
Basi la UDA lenye namba za usajili T
696 CVP limegonga treni katika eneo la Kamata Jijini Dar es Salaam usiku wa
kuamkia leo, July 27,2016, wakati Basi hilo likotokea
stendi ya Gerezani, Kariakoo kuelekea Mbagala na kuua mtu mmoja na wengine zaidi
ya 45 kujeruhiwa.
Kaimu Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa
Kipolisi wa Ilala, Ernest Matiku amesema majeruhi wamepelekwa Hospitali ya
Taifa ya Muhimbili kwa matibabu.
Hata hivyo, hakuweza kumtaja jina mtu
huyo aliyefariki dunia.
“Ni kweli ajali imetokea kuna kifo
cha mtu mmoja na watu wengi wameumia sana ,” amesema Kaimu kamanda huyo.
|
No comments:
Post a Comment