|
Mikoa itakayonufaika
katika awamu ya kwanza ya ugawaji wa madawati hayo ni Dar es salaam, Pwani,
Morogoro, Lindi, Mtwara, Ruvuma, Iringa, Njombe, Mbeya, Songwe, Rukwa, Katavi,
Unguja, Pemba na Tanga.
Akizungumza katika
hafla hiyo, Rais Magufuli amesema baada ya kuanza kutekeleza ahadi ya kuondoa
ada kwa shule za msingi na sekondari, idadi ya wanafunzi waliojiandikisha
kuanza darasa la kwanza imeongezeka kutoka wanafunzi 1,282,100 hadi kufikia
wanafunzi 1,896,584 sawa na ongezeko la asilimia 84.5 hali iliyosababisha
upungufu wa madawati 1,400,000 lakini tatizo hilo limetatuliwa kwa kiasi
kikubwa ambapo mpaka sasa zaidi ya madawati 1,000,000 yametengenezwa.
Aidha, Dkt. Magufuli
amelitaka Jeshi la Kujenga Taifa (JKT) na Jeshi la Magereza kuongeza kasi
katika utengenezaji wa madawati ili yakamilike haraka na kuanza kutumika.
|
|
Rais wa John Magufuli
na Mbunge wa Ilala Mussa Azzan Zungu ambaye aliyapokea madawati kwa niaba ya
Wabunge wa majimbo mbalimbali nchini.
|
|
Rais John Pombe
Magufuli na Wanafunzi wa shule ya msingi Bunge
|
|
Rais Magufuli na Mbunge
wa Iringa Mjini mchungaji Peter Msigwa.
|





No comments:
Post a Comment