|
Kaimu Mrajisi wa Vyama
Vya Ushirika Nchini Dkt. Audax Peter Rutabanzibwa.
Dkt. Rutabanzibwa
alisema baada ya kutuma wakaguzi kutoka ofisi ya Mrajisi wa Vyama vya Ushirika
nchini, Wakaguzi hao walibaini kuwa taarifa waliyosomewa wananchama katika
mkutano ilitaja kuwa deni lilikuwa Shilingi bilioni 2.8 kumbe haikuwa kweli
kwani deni lilikuwa limepanda hadi shilinngi bilioni 3.15 Bodi na Meneja Mkuu
walikuwa wamewadanganya wanachama wa
chama hicho.
Pili, Wakaguzi hao waligundua kuwa shilingi Milioni
124 zilitumika katika malipo na hakukuwa na maelezo ya kutosheleza kuhusu
malipo ya fedha hizo.
Tatu, KCU iliingia mikataba ya kukodisha majengo
yake amabayo haikufuata bei ya soko kwa sasa, na
mikataba hiyo ilifungwa kwa makubaliano ya miaka 10 jambo ambalo linapelekea
Chama hicho kulipwa pango kwa bei ya chini kabisa isiyoendana na soko.
Nne, Chama Kikuu cha
Ushirika Mkoani Kagera KCU kimekuwa kikinunua kahawa ya kiwango cha chini
kabisa na kusababisha hasara kubwa. Tano, Chama cha KCU kilijiingiza kataika
miradi isiyokuwa na tija kama mradi wa kununua maharage ambao ulikisababishia
hasara kubwa Chama hicho.
Dkt. Rutabanzibwa
alisema kuwa kutokana na sheria Na. 6 ya mwaka 2003 inayohusu usimamizi wa
Vyama vya Ushirika nchini Bodi ya KCU hakufanya kazi yake ipasavyo ya
kukisimamia vizuri chama hicho Aidha, Bodi hiyo ilifanya vikao 12 kwa mwaka
jana 2015 vikao ambavyo vinaonekana havikuwa na tija kwani pamoja na vikao
hivyo vya Bodi kufanyika bado kulikuwa na ubadhirifu mkubwa wa fedha.
MAELEKEZO.
Dkt.
Ruatabazibwa baada ya kutaja ubadhirifu uliofanyika katika Chama Kikuu cha
Ushirika KCU alisema kuwa Serikali imeamua kuchuka hatua zifuatazo;-
1. Kufuta Bodi ya Chama Kikuu cha
Ushirika Mkoani Kagera KCU iliyoteuliwa mwaka 2014.
2. Kusitisha ajira ya Meneja Mkuu wa KCU
Bw. Vedastus Ngaiza mpaka hapo uchunguzi wa tuhuma za ubadhirifu wa fedha
utakapokamilika.
3. Kusitisha nafasi ya Mrajisi Msaidizi
wa Mkoa wa Kagera Bw. Nestory Shorozi kwani ubadhirifu huo ulifanika yeye
akiwepo bila kukishauri vizuri Chama
hicho Kikuu cha Ushirika .
4. Akaunti zote za Chama cha Ushirika
KCU kusimamishwa mara moja mpaka hapo utaratiibu mzuri utakapokuwa umewekwa .
KUNUSURU CHAMA.
Dkt. Rutabanzibwa alisema kuwa katika kukinusuru Chama Kikuu cha KCU pia
na kuendelea na Msimu wa manunuzi ya kahawa Serikali imefanya uteuzi mdogo wa Mrajisi
Msaidizi Bw, Robert Makene Mtambo kutoka Ukerewe Mkoani Mwanza atakayeshikiria kwa muda nafasi ya Bw.
Nestory Shorozi aliyekuwa Mrajisi Msaidizi wa Mkoa wa Kagera.
Aidha mrajisi Msaidizi aliyeteuliwa Bw. Mtambo atakaimu nafasi ya Meneja Mkuu wa KCU
iliyokuwa ikishikiliwa na Bw. Vedastus Ngaiza.
Katika kukaimu nafasi hiyo Bw.
Mtambo atatakiwa kuitisha Mkutano Mkuu wa wanachama wa KCU ndani ya mwezi
mmoja na katika mkutano huo atateuliwa
Mwenyekiti ambaye atatakiwa kusoma taarifa halisi ya KCU iliyotakiwa kusomwa mwezi
Mei 2016 katika Mkutano Mkuu.
Adha Dkt. Rutabanzibwa alisema Serikali haikukurupuka
kuchukua hatua hiyo bali ilifanya uchunguzi wa kutosha ikiwa ni pamoja kuipa
bodi nafasi ya kujieleza lakini haikutoa maelezo ya kutosha na badala ya
kupunguza deni wao waliliongeza deni likapanda zaidi.
Pia Dkt. Rutabanzibwa
aliviagiza vyombo vya uchunguzi kama TAKUKURU, Polisi na Usalama kuanza
kulifanyia kazi suala hilo mara moja.
Kaimu Mrajisi wa Vyama Vya Ushirika Dkt. Audax Peter
Rutabanzibwa alimalizia kwa kusema kuwa Serikali imeamua kulifanyia kazi suala
la VyamaVikuu vya Ushirika nchini kwani vyama hivyo vimeonekana kuwa badala ya
kuwasaidia wakulima vinawadidimiza ambapo alisema walianzia Mwanza, sasa
Kagera, na wanaelekea Mikoa ya Geita, Simiyu, na Shinyanga.
|
No comments:
Post a Comment