Uzimaji wa
Imei bandia ulifanyika usiku wa kuamkia jana kwa Mamlaka ya Mawasiliano
Tanzania (TCRA) katika simu zaidi ya 600,000 zenye IMEI batili.
Kwa mujibu
wa TCRA, IMEI ni namba ya kimataifa ya utambuzi wa vifaa vya kielektroniki,
ikiwamo simu. Ina tarakimu 15 ambazo ni za kipekee kwa kifaa husika na
zinatambulika kimataifa. Namba hizo hutumika kudhibiti bidhaa bandia au simu
kutumiwa na mtu mwingine.
Jana,June 17,2016, Mkurugenzi wa Kitengo cha Mawasiliano wa TCRA, Bw.Innocent Mungy alisema takwimu
hizo ni zile ambazo zimetokana na kazi ya kukata mawasiliano katika simu bandia
iliyofanyika kuanzia saa sita usiku mpaka saa kumi alfajiri ya jana.
Alisisitiza
kuwa mtambo huo unaendelea na kazi kuhakikisha kuwa hata simu ambazo hazipo au
hazikuwa hewani zitakapowashwa hazitafanya kazi.
“Kazi ya
kuzima simu hizo ilianza usiku wa kumkia jana saa sita usiku na kila kampuni ya
mtandao wa simu ilipaswa kuzima simu za wateja wake ambazo ni feki na kazi ya
mtambo ni kuhakikisha simu iliyozimwa inapowekewa kadi ya mtandao mwingine
haifanyi kazi na kuhakikisha simu zote feki zitakazoingia nchini hazifanyi
kazi,” alisema
Mungy.
Hata hivyo,
kuna baadhi ya wamiliki wa simu ambao walitilia shaka ufanisi wa mtambo huo kwa
madai kuwa tayari walishathibitishiwa na TCRA kwamba simu zao ni feki, lakini
bado zinafanya kazi.
“Simu
yangu mimi niliangalia nikaambiwa ni feki na niibadilishe kabla ya tarehe 16
Juni,2016, lakini jana wamezizima feki ya kwangu bado inafanya kazi kama kawaida
napiga na kupokea simu kama zamani,”alisema Nael Joseph.
Kuhusu suala hilo, Mungy alisema: “Hoja hizo zimejitokeza kwa wingi na
wengine walifikia hatua ya kuushutumu mtambo wetu kuwa ni feki na kuwa
umeshindwa kuzima simu feki ukazima orijino, lakini ukweli ni kwamba mtambo ule
hauzimi kama taa au kama ule uliozima matumizi ya analojia bali unazima
taratibu.
"Niweke sawa kwamba mtambo huu hauonei mtu na unazima simu zote zilizo
feki.”
Mungy aliongeza kuwa wengi wamekuwa hawaelewi mantiki ya ujumbe wa
uthibitisho.
Alisema ujumbe unamtaka mmliki wa simu kuoanisha jina linalotajwa
kama ndilo jina halisi la simu yake. “Kama jina linalotajwa na Imei
linaoana na lililoandikwa kwenye simu yako, basi sio feki, lakini majina yakiwa
hayafanani ndipo simu inakuwa feki,” alifafanua.
VODACOM
WAZUNGUMZA.
Mkurugenzi wa Mawasiliano wa Vodacom, Bw.Rosalynn Mworia alisema walipewa jukumu
la kuzima simu feki za wateja wao na TCRA.
“Jana saa
sita usiku tulitekeleza agizo kama lilivyotolewa na TCRA na inavyoonekana wengi
wao walikuwa wamejipanga kwani simu nyingi zimezimwa, lakini baadhi wamerejea
hewani japokuwa wapo ambao mpaka sasa hawajarudi,” alisema Mworia .
|
No comments:
Post a Comment