TASWIRA PICHA:-Namna Jengo La NSSF - Akiba Lawaka Moto. - Mwana Wa Makonda

Muhtasari

X-BET


Post Top Ad

Saturday, May 07, 2016

TASWIRA PICHA:-Namna Jengo La NSSF - Akiba Lawaka Moto.

Jengo la NSSF la eneo la Akiba jijini Dar es Salaam Jana,May 06,2016,majira ya jioni limeshika moto ambao kwa bahati nzuri Jeshi la Zimamoto liliwahi kufika eneo la tukio na kuudhibiti.  Chanzo cha moto huo kinasemekana ni kulipuka kwa mtungi wa gesi katika moja ya vyumba vya ghorofa ya juu katika jengo hilo liitwalo Akiba House.

Magari ya Jeshi la Zimamoto yakiwa eneo la tukio Kuzima moto huo katika jengo la NSSF  lililopo eneo la Akiba jijini Dar es Salaam muda huu. 

Moto huo inasemekana hakuna madhara makubwa (ya kibinadamu) yaliyojitokeza baada ya Jeshi la Zimamoto kufika kwa wakati katika eneo hilo.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad