SHEREHE YA WAFANYAKAZI TANZANIA:- TAMISEMI yaongoza kwa Watumishi Hewa Hadi Jana May 01, 2016. - Mwana Wa Makonda

Muhtasari

X-BET


Post Top Ad

Monday, May 02, 2016

SHEREHE YA WAFANYAKAZI TANZANIA:- TAMISEMI yaongoza kwa Watumishi Hewa Hadi Jana May 01, 2016.

Sehemu ndogo ikionesha wafanyakazi waliojitokeza katika Uwanja wa Jamhuri mkoani Dodoma katika kilele cha sherehe za Siku ya Wafanyakazi Duniani zilizofanyika Kitaifa Jana May 01, 2016,Mkoani Dodoma. 

PICHA NA IKULU.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dr. John Pombe Magufuli  ametangaza kushusha kodi ya mapato ya Mshahara ( Pay as you Earn -PAYE  )  kutoka asilimia 11 iliyopo sasa hadi asilimia 9.

Rais Magufuli,amesema ameamua kuchukua umamuzi huo ili kutimiza ahadi yake aliyoitoa wakati wa kampeni ya kuwapunguzia mzigo wafanyakazi kwa kuwaongezea mishahara na kuwapunguzia kodi ya mapato ya mishahara.

Kuhusu kuwaongezea mishahara, Rais Magufuli ameomba wafanyakazi wamvumilie kwa kuwa hivi sasa yuko kuimarisha uchumi wa nchi kwa kuziba mianya yote ya Rushwa.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiwahutubia mamia ya Wafanyakazi katika kilele cha Maadhimisho ya Sherehe za Siku ya Wafanyakazi Duniani zulizofanyika Kitaifa katika Uwanja wa Jamhuri mkoani Dodoma.

Katika hatua nyingine, Rais Magufuli amewataka waajiri wote nchini kuwapa wafanyakazi wao mikataba ya ajira na kupeleka makato yao kwenye mifuko ya hifadhi ya jamii bila kukosa.

Pia amesema kuwa Idadi wa watumishi hewa nchini  imeendelea kuongezeka ambapo takwimu za hadi jana,May 01, 2016 zinaonyesha kuwepo kwa watumishi hewa 10,295.

Akihutubia wakati wa maadhimisho ya sherehe za Mei Mosi,  Rais  wa Jamhuri ya Muungano ya Tanzania  Dr John Pombe Magufuli amesema kati ya watumishi hao hewa, 8,373  wanatoka  TAMISEMI   na watumishi 1.922 wanatoka SERIKALI KUU.

Amesema watumishi hao walikuwa wakiligharimu taifa sh. Bilioni 11.6 kwa mwezi sawa na Bilioni 139  kwa  mwaka.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad