BUNGENI DODOMA:- Wabunge Wanawake UKAWA watoka nje ya Bunge baada ya Mbunge wa CCM Kuwatuhumu Kwamba Wamepata Ubunge Kwa Kufanya Mapenzi na Viongozi Wao. - Mwana Wa Makonda

Muhtasari

X-BET


Post Top Ad

Friday, May 06, 2016

BUNGENI DODOMA:- Wabunge Wanawake UKAWA watoka nje ya Bunge baada ya Mbunge wa CCM Kuwatuhumu Kwamba Wamepata Ubunge Kwa Kufanya Mapenzi na Viongozi Wao.

Wabunge Wanawake wa Upinzani wametoka wote nje ya Bunge kwa madai ya kudhalilishwa bungeni na Mbunge wa jimbo la Ulanga Goodluck Mlinga (CCM ) aliyedai jana kuwa viti maalum Ukawa hutolewa kwa rushwa ya ngono.

Mlinga alitoa kauli hiyo Jana,Al hamis,May 05,20165,wakati akichangia hotuba Wizara ya Katiba na Sheria  ambapo alisema ili uweze kuwa mbunge wa viti maalum chadema, lazima ufanye mapenzi na kiongozi wako wa chama.

Wabunge hao leo asubuhi  waliomba mwongozo kwa Naibu Spika kupitia kwa Mbunge Sophia Mwakagenda wa viti maalumu (Chadema)kumtaka mbunge huyo athibtishe kauli yake  lakini hawakusikilizwa na badala yake Naibu spika aliwataka wakae chini.

Baada ya mabishano ya dakika kadhaa pasi kusikilizwa, wabunge hao walisimama wote na kuamua kutoka nje  ya ukumbi wa bunge huku wakiahidi kuja na tamko kali kuhusu udhalilishaji waliofanyiwa.......HAPA BOFYA ………..==>Msikilize hapa Mbunge wa Kawe na Mwenyekiti wa Umoja wa Wanawake CHADEMA, Halima Mdee akizungumza na waandishi wa habari nje ya ukumbi wa Bunge mjini Dodoma, baada ya wabunge hao kutoka nje

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad