![]() |
|
Wafanyabiashara
wengi katika soko hilo wamesikitishwa na kutokea kwa janga hilo, kwani wengi
wao wamesema walikuwa na mikopo na hawakuwa na bima ya mali zao.
Jonasi
Nyarugenda ni miongoni mwa wafanyabiashara hao anasema “Moto umeteketeza stoo zangu nne zenye bidhaa
mbalimbali kama sukari, mchele, ngano na mafuta, kwakeli ukitathimini kwa
haraka siyo chini ya milioni 45 zimepotea.”
Amesema
kwamba alikuwa hana bima katika mkopo wake wa milioni 20 kutoka katika Benki.
|
![]() |
|
Hasara hiyo
kwa kiasi kikubwa imechangiwa na ukosefu wa vifaa vya kuzima moto.
Wananchi wa
Karagwe imewapasa kusubiri gari la Zimamoto kutoka Bukoba Mjini (magari ya
uwanja wa ndege) ambako ni kilomita 120 mpaka kufika karagwe mjini.
Hata hivyo
magari hayo yalikuta maduka mengi katika soko hilo yamekwishateketea.
Diwani wa
kata ya Kanoni wilayani Karagwe, Mhe Sabi Rwazo amesema tukio hilo limewashtua na
ni tukio la kwanza la moto kuunguza soko wilayani humo.
Anasema
tatizo la ukosefu wa gari la zima moto linachangiwa na uhaba wa fedha.
“Mara nyingi
katika bajeti yetu imekuwa ikishindwa kununua gari.” Amesema Rwazo na kusema
maombi yao yako serikali kuu.
|


![]() |
|
Mkuu wa
Wilaya ya Karagwe Deodatus Kinawiro amesema kuwa serikali ya wilaya yake iko katika mchakato wa kupata gari la zima moto hivi karibuni,
“Bahati
nzuri nilikuwa Dar es Salaam, nimekutana na kamishna mkuu wa zima moto
ameniahidi kunipatia gari jipya,” amesema Kinwiro na kuongeza kuwa, “wakati
wowote gari hilo litafika wilayani Karagwe.”
Hata hivyo
baadhi ya Wananchi wanasema hawakubaliani na kauli hiyo ya mkuu wa wilaya kwa
sababu wamekuwa wakitozwa kiasi cha TZS 30,000 kwa mwezi ili kuchangia huduma
za zimamoto wilayani hapo lakini wanashangaa kwa nini hawapati elimu ya
kujikinga na majanga, na hakuna hata gari la dharura.
Mpaka sasa
chanzo cha moto huo hakijajulikana lakini taarifa za awali zimeonesha kuwa kuna
Mamalishe mwenye kibanda sokoni hapo aliacha jiko lake bila kuzima hivyo likashika
nguo zilizokuwa katika kibanda hicho na kusababisha moto kusambaa ghafla.
|








No comments:
Post a Comment