MAAMBUKIZI YA UKIMWI KAGERA:-Wilaya ya Bukoba vijijini yaongoza mkoani Kagera kwa asilimia 6.0...Ngara kwa asilimia 2.3. - Mwana Wa Makonda

Muhtasari

X-BET


Post Top Ad

Tuesday, February 23, 2016

MAAMBUKIZI YA UKIMWI KAGERA:-Wilaya ya Bukoba vijijini yaongoza mkoani Kagera kwa asilimia 6.0...Ngara kwa asilimia 2.3.

WATU elfu 18 na 887 sawa  na asilimia 4 wamekutwa na  maambukizi ya Virusi vya UKIMWI, kati ya watu  Laki 4, elfu 77 na 493 ambao  walijitokeza  kupima virusi vya Ukimwi kwa hiari  katika mkoa wa  Kagera  kwa mwaka 2015 / 2016.  

Afisa Maendeleo ya Jamii mkoani Kagera ,Bw Charles Mafyimbo amesema hayo wakati akiongea na Wanahabari, ofisini kwake juu  hali ya maambukizi ya virusi vya Ukimwi ilivyo kwa sasa katika mkoa wa Kagera.

Amesema  katika wilaya  za mkoa wa Kagera, wilaya  ya Bukoba vijijini inaogoza kwa maambukizi  ya virusi vya UKIMWI kwa kuwa na asilimia 6.0  ikifuatia  na  wilaya  ya Muleba   ambayo ina asilimia 5.5  huku Manispaa ya Bukoba  ikiwa na asilimia 4.6  na kwamba wilaya ya  Ngara maambukizi  ya virusi vya ukimwi yameshuka   kwa asilimia 2.3 tofauti na mwaka 2014 ilikuwa asilimia2.6.

Hata hivyo Bw  Mafyimbo  amesema elimu inaendelea kutolewa kwa  Jamii huku akitaja  wilaya zinazongoza kwa maabukizi ya ukimwi  zina mwingiliano  wa watu wakiwemo  kutoka Visiwani ,Bandarini ikiwemo Kemondo na maeneo ya mipakani ya Kabanga,Rusumo wilayani Ngara na Mtukula  wilayani Misenyi.


Pata Picha, Habari za  Siasa, Kijamii, Biashara, Muziki na Michezo na Nyingine kwa kujiunga  na Mimi Hapa...FACEBOOK .. TWITTER .. INSTAGRAM … Pia Usisite kututumia tukio la Picha/Habari  kwa WhatsApp +255789925630  Or  +255756830214.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad