KOMBE LA SHIRIKISHO:-Yanga SC yashinda 2-1…VPL:-Azam FC sare..! - Mwana Wa Makonda

Muhtasari

X-BET


Post Top Ad

Wednesday, February 24, 2016

KOMBE LA SHIRIKISHO:-Yanga SC yashinda 2-1…VPL:-Azam FC sare..!


Leo,February 24,2016,Mjini  Sokoine Jijini Mbeya katika Mechi ya Ligi Kuu Vodacom Tanzania bara 2015/2016 ,Timu ya Tanzania Prisons ilitoka Sare 0-0 na Azam FC  wakati Jijini Dar es Salaam kwenye Mechi ya Kombe la Shirikisho ikiwa ni Raundi ya Mtoano ya Timu 16, Yanga iliwachapa JKT Mlale Bao 2-1.

Kwenye VPL, Sare ya Azam FC imewabakisha Nafasi ya Pili licha ya kuwakamata Vinara Yanga kwa Pointi, wote wakiwa na Pointi 46 kwa Mechi 19 kila mmoja, lakini Yanga wanabakia kileleni kwa ubora wa Magoli.

Simba SC wanaendelea kushika Nafasi ya 3 wakiwa Pointi 1 nyuma lakini wao wamecheza Mechi 1 zaidi.

Katika Mechi ya Yanga SC na JKT Mlale, Yanga SC walitoka nyuma kwa Bao 1 na Paul Nonga na Thaban Kamusoko kuwafungia Bao zao huko mpishi wa Bao zote akiwa Geofrey Mwashiuya.

Ushindi huu umewaingiza Yanga SC hatua ya Robo Fainali ya Kombe la Shirikisho.

KOMBE LA SHIRIKISHO



Raundi ya 4



Ratiba/Matokeo



Jumatano Februari 24,2016.

Yanga SC 2 - 1 JKT Mlale

Ijumaa Feb 26,2016.

Ndanda FC v JKT Ruvu

Coastal Union v Mtibwa Sugar

Jumamosi Feb 27,2016.
Mwadui FC v Rhino Rangers

Tanzania Prisons v Mbeya City

Jumapili Feb 28,2016.

Panone FC v Azam FC (Ushirika, Moshi)

Simba SC v Singida United

Toto Africans v Geita Gold

 Pata Picha, Habari za  Siasa, Kijamii, Biashara, Muziki na Michezo na Nyingine kwa kujiunga  na Mimi Hapa...FACEBOOK .. TWITTER .. INSTAGRAM … Pia Usisite kututumia tukio la Picha/Habari  kwa WhatsApp +255789925630  Or  +255756830214.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad