Messi
amefunga mabao hayo dakika ya 71 akimalizia pasi ya Neymar wakati la pili
alifunga kwa penalti dakika ya 83, baada ya yeye mwenyewe kuangushwa na Mathieu
Flamini.
Arsenal sasa
watalazimika kupanda mlima katika mchezo wa marudiano mwezi ujao Uwanja wa Camp
Nou kwa kushinda 3-0 ili kwenda Robo Fainali.
|
|
Katika
mchezo mwingine,Juventus wakiwa nyumbani dhidi ya Buyern Munich, mchezo huo
umemalizika kwa timu hizo kutoshana nguvu kufuatia sare ya kufungana mabao 2-2.
Bayern
Munich ndio walioanza kuzigusa nyavu za wapinzani kwa kuandika bao la kuongoza
kupitia kwa mchezaji wao Thomas Muller dakika ya 43, muda mchache baadaye Arjen
Robben akaandika bao la pili kwa buyen Munich katika dakika ya 55 kipindi cha
pili.
|
|
Kwa upande
wao Juventus walizinduka na kuandika bao la kwanza kupitia kwa Paulo Dybala
ikiwa ni dakika ya 63 kipindi cha pili, huku Stefano Sturaro akiandika bao la
pili la kusawazisha dakika ya 76 na kuufanya mchezo umalizike kwa sare ya
kufungana bao 2-2.
Bayern sasa
wanaweza kusonga mbele hata kwa sare ya 0-0 au 1-1 katika mchezo wa marudiano
Ujerumani, kwani watanufaika na sharia ya mabao ya ugenini.
Michuano
hiyo itaendelea tena Jumatano kwa Mechi 2 Dynamo Kiev ikiikaribisha Man City
huko Ukraine na PSV Eindhoven wao watakuwa Wenyeji huko Uholanzi dhidi ya
Atletico Madrid.
|





No comments:
Post a Comment