|
Rais Robert
Mugabe wa Zimbabwe ambaye alizaliwa February 21,1924,ametimiza umri wa miaka 92
huku chama chake kikisema atawania tena Urais 2018.
Mnadhimu
wake mkuu alisema kiongozi huyo ambaye ameongoza nchi tangu mwaka 1980, bado
ana uwezo kamili wa kuongoza Serikali licha ya tetesi kwamba hawezi kuongoza
kutokana na umri.
Akizungumza
na gazeti la Serikali Sunday Mail, Katibu Mkuu wa Rais,Bw. Misheck Sibanda alisema
tetesi hizo si za kweli na hazina msingi kwani Mugabe ana ratiba ya wiki nzima
kutekeleza kazi za Serikali na chama.
Rais Mugabe
ambaye aliapa kuongoza nchi hadi atakapokufa, alishinda kipindi kingine cha
urais cha miaka mitano kwenye uchaguzi wa mwaka 2013 uliofanyika chini ya
katiba mpya inayoweka ukomo wa kuongoza kwa vipindi viwili tu vya miaka mitano.
Chama chake
tayari kimetangaza kumpitisha Mugabe kama mgombea Urais katika uchaguzi wa
mwaka 2018.
Mugabe
amekua kiongozi wa Zimbabwe tangu 1980. Ni mwenyekiti wa chama tawala cha Zanu.
1980 alikuwa waziri mkuu na 1987 Rais wa Zimbabwe.
Utawala wa
Mugabe umeitwa wa kidikteta tangu mwaka 2002 kutokana na kudharau haki za binadamu nchi Zimbabwe.
Pata Picha, Habari za Siasa, Kijamii, Biashara, Muziki na Michezo na Nyingine kwa kujiunga na Mimi Hapa...FACEBOOK .. TWITTER .. INSTAGRAM … Pia Usisite kututumia tukio la Picha/Habari kwa WhatsApp +255789925630 Or +255756830214.
|
No comments:
Post a Comment