EPL 2015/2016:-Aston Villa 0-6 Liverpool ....Arsenal 2-1 Leicester..Matokeo Mechi za leo February 14. - Mwana Wa Makonda

Muhtasari

X-BET


Post Top Ad

Sunday, February 14, 2016

EPL 2015/2016:-Aston Villa 0-6 Liverpool ....Arsenal 2-1 Leicester..Matokeo Mechi za leo February 14.


Liverpool wamepata mteremko huko Villa Park baada ya kuwanyuka Aston Villa Bao 6-0 katika Mechi ya Ligi Kuu Uingereza ,leo February 14,2016.

Hadi Mapumziko, Liverpool walikuwa mbele kwa Bao 2-0 zilizofungwa na Daniel Sturridge na James Milner katika Dakika za 16 na 25 na Kipindi cha Pili kuongeza Bao 4 zaidi kupitia Can, Dakika ya 58, Origi,63, Clyne, 65, na Kolo Touré, 71.
Ushindi huu umewapandisha Liverpool na kukamata Nafasi ya 8 wakati Aston Villa wanabaki mkiani kabisa.
Nao wakiwa kwao Emirates, Arsenal , wametoka nyuma kwa Bao 1-0 na kuwafunga Mtu 10 Leicester City Bao 2-1.

Ushindi huu umewafikisha Arsenal Pointi 51 wakiwa Pointi 2 nyuma ya Vinara Leicester na sasa wako Nafasi ya Pili lakini wanaweza kushushwa baadae Leo ikiwa Tottenham itaifunga Manchester City huko Etihad.
Jamie Vardy alifunga Penati ya Dakika ya 45 baada ya yeye mwenyewe kuchezewa rafu na kuangushwa na Monreal na kuipa Leicester Bao la kuongoza.

Kipindi cha Pili Dakika ya 54, Leicester walibaki Mtu 10 baada ya Simpson kupewa Kadi ya Njano ya Pili kwa kumvuta Mkono Giroud na hivyo kuonyeshwa Kadi Nyekundu.

Dakika ya 70 Arsenal walisawazisha Bao kupitia Theo Walcott huku bao la ushindi kwa Arsenal lilifungwa na Danny Welbeck, Mchezaji ambae alikuwa Majeruhi tangu Aprili Mwaka Jana 2015.


Pata Picha, Habari za  Siasa, Kijamii, Biashara, Muziki na Michezo na Nyingine kwa kujiunga  na Mimi Hapa...FACEBOOK .. TWITTER .. INSTAGRAM … Pia Usisite kututumia tukio la Picha/Habari  kwa WhatsApp +255789925630  Or  +255756830214.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad