Makamu
Mwenyekiti wa Shirika la Kimataifa la ActionAid nchini, Dkt. Azaveli
Lwaitama akitoa neno la ufunguzi wakati wa warsha ya uzinduzi wa mradi
wa kuimarisha elimu kupitia vyanzo vya ndani vya mapato (Promoting
Quality Education Through Progressive Domestic Resource
Mobilization).(Picha na Modewjiblog).
Katika
kusaidia uboreshwaji wa elimu ya Tanzania, Shirika la Kimataifa la
ActionAid kwa kushirikiana na serikali ya Norway kupitia Wakala wa
Maendeleo na Ushirikiano (NORAD) wamezindua mradi kuimarisha elimu
kupitia vyanzo vya ndani vya mapato (Promoting Quality Education Through
Progressive Domestic Resource Mobilization).
Akielezea
kuhusu mradi huo, Makamu Mwenyekiti wa ActionAid nchini, Dkt. Azaveli
Lwaitama alisema mradi huo unataraji kusaidia uboreshwa wa elimu nchini
na zaidi maeneo ya vijijini sehemu ambapo zimekuwa zikionekana kuwa
nyuma kielemu.
Alisema
ili kupatikana kwa elimu bora kunahitajika uwekezaji wa kuboresha elimu
kwa maeneo yote yanayohusika na elimu na inatakiwa kuanza na elimu ya
shule ya msingi ili kuweza kumwandaa mwanafunzi kuanzia akiwa mdogo kwa
kupata elimu bora inayokidhi viwango vya kimataifa.
“Elimu
bora inataka kuwepo kwa uwekezaji kuanzia kwenye shule za msingi kwa
kila jambo kama ni uniform, kalamu, uji, walimu kupatiwa stahiki zao na
mengine yote yatimizwe,
“Ukitaka
elimu bora lazima ujue inahitaji uwekezaji na mradi huu unataka
kuongeza fursa kwa wanafunzi kwa kuanzia shule za msingi na zaidi
tunaangalia vijijini,” alisema Dkt. Lwaitama.
Nae
mgeni rasmi katika uzinduzi wa mradi huo, Balozi wa Norway nchini,
Hanne-Marie Kaarstad alisema Norway na Tanzania wamekuwa wakishirikiana
katika shughuli mbalimbali za maendeleo na ana furaha kuona mradi huo
unafanyika kwa maendeleo ya baadae ya Tanzania.
Alisema
Norway itaendelea kusaidia miradi mbalimbali ya elimu nchini katika
kusaidia vijana kupata elimu kuanzia ngazi ya msingi hadi vyuo vya
ufundi ili kuweza kuongeza wasomi ambao watasaidia ukuaji wa uchumi
nchini.
“Nina
furaha kuona mradi ambao utakuwa na mambo muhimu kwa ajili ya maendeleo
ya sasa na baadae kwa Tanzania ninataraji kuona miradi inafanikiwa na
ushirikiano wa Norway na Tanzania kwa miaka 50 sasa unazidi kuimarika na
Tanzania inaushirikiano mzuri na Norway,” alisema Kaarstad.
Kwa
upande wa Paul Mikongoti kutoka Kituo cha Sheria na Haki za Binadamu
alisema kupitia Katiba ya Tanzania ya mwaka 1977, ibara ya 11 (2)
inaeleza kuwa kila Mtanzania anayo haki ya kujielimisha na kusoma ngazi
zote za elimu hadi anapoamua kuacha kuendelea kusoma na hivyo mradi huo
utasaidia watanzania kupata haki yao ya kikatiba.
Mradi
huo unataraji kufanyika katika wilaya za Kilwa na Singida na utakuwa wa
miaka mitatu ambao unataraji kuzifikia shule 60, 30 kwa kila wilaya.
Aidha
unataraji kuwafikia wanafunzi wa kiume 7,758 na wakike 8,474 kwa wilaya
ya Singida na Kilwa kuwafikia wanafunzi wa kiume 6,607 na wakike 6,546
lakini pia walimu 287 kwa Singida na 290 kwa Kilwa.
Baadhi ya wadau wa sekta ya elimu walioshiriki katika warsha ya uzinduzi wa mradi wa kuimarisha
elimu kupitia vyanzo vya ndani vya mapato (Promoting Quality Education
Through Progressive Domestic Resource Mobilization).
Kaimu Mkurugenzi Mkazi wa Shirika la ActionAid, Josaphat Mshighati akitoa maelezo kuhusu mradi wa kuimarisha
elimu kupitia vyanzo vya ndani vya mapato (Promoting Quality Education
Through Progressive Domestic Resource Mobilization).
Mshereheshaji
wa warsha ya uzinduzi wa mradi wa kuimarisha elimu kupitia vyanzo vya
ndani vya mapato (Promoting Quality Education Through Progressive
Domestic Resource Mobilization), Jovina Nawenzake akisherehesha wadau wa
sekta ya elimu waliohudhuria uzinduzi huo.
Kalistus
Chonya kutoka Ofisi ya Sera katika Wizara ya Elimu, Sayansi, Teknolojia
na Ufundi akielezea kuhusu sera ya elimu inayotumika nchini na mipango
waliyonayo ili kuiboresha zaidi.
Paul Mikongoti kutoka Kituo cha Sheria na Haki za Binadamu akielezea kuhusu haki ya elimu kwa watanzania.
Samwely Mkwatwa kwa niaba ya AAT akielezea kuhusu jinsi kodi inavyoweza kusaidia ukujuaji wa elimu Tanzania.
Balozi
wa Norway nchini, Hanne-Marie Kaarstad akifurahia jambo wakati wa
uzinduzi wa mradi kuimarisha elimu kupitia vyanzo vya ndani vya mapato
(Promoting Quality Education Through Progressive Domestic Resource
Mobilization).Kulia ni Makamu Mwenyekiti wa Shirika la Kimataifa la
ActionAid nchini, Dkt. Azaveli Lwaitama.
Balozi wa Norway nchini, Hanne-Marie Kaarstad akisoma hotuba wakati wa uzinduzi wa mradi wakuimarisha
elimu kupitia vyanzo vya ndani vya mapato (Promoting Quality Education
Through Progressive Domestic Resource Mobilization). Kushoto ni Makamu
Mwenyekiti wa Shirika la Kimataifa la ActionAid nchini, Dkt. Azaveli
Lwaitama.
Baadhi ya wahuzuriaji waliohudhuria katika warsha ya uzinduzi wa mradi wa kuimarisha
elimu kupitia vyanzo vya ndani vya mapato (Promoting Quality Education
Through Progressive Domestic Resource Mobilization) iliyoandaliwa na
Shirika la ActionAid.
Balozi wa Norway nchini, Hanne-Marie Kaarstad akizindua taarifa kuhusu mradi wa kuimarisha
elimu kupitia vyanzo vya ndani vya mapato (Promoting Quality Education
Through Progressive Domestic Resource Mobilization).
Balozi
wa Norway nchini, Hanne-Marie Kaarstad akimkabidhi taarifa ya mradi wa
kuimarisha elimu kupitia vyanzo vya ndani vya mapato (Promoting Quality
Education Through Progressive Domestic Resource Mobilization), Kalistus
Chonya kutoka Ofisi ya Sera katika Wizara ya Elimu, Sayansi, Teknolojia
na Ufundi.
Kwa pamoja wakionyesha taarifa hiyo kwa wahudhuriaji wa warsha hiyo.
Watekelezaji
wa mradi wa kuimarisha elimu kupitia vyanzo vya ndani vya mapato
(Promoting Quality Education Through Progressive Domestic Resource
Mobilization), wakisaini mikataba na mwongozaji wa mradi huo.
Mkuu
wa Elimu kwa Mlipakodi kutoka Mamlaka ya Mapato nchini (TRA), Patrick
Ezekiel akielezea kuhusu jinsi kodi inavyoweza kusaidia kuinua elimu
nchini.
Mratibu Mkuu wa TEN/MET nchini, Cathlee Sakwambo akitoa neno la ufungaji wa warsha ya uzinduzi wa mradi wa kuimarisha
elimu kupitia vyanzo vya ndani vya mapato (Promoting Quality Education
Through Progressive Domestic Resource Mobilization).
Washiriki wakiwa katika picha ya pamoja.





No comments:
Post a Comment