TAARIFA KWA
VYOMBO VYA HABARI WAZIRI MKUU AFURAHISHWA NA HALI YA CHAKULA MKOANI RUVUMA
WAZIRI MKUU
Kassim Majaliwa amefurahishwa na hali ya chakula mkoani Ruvuma, ikiwa kati ya
mikoa inayotegemewa kwa uzalishaji wa chakula kwa wingi nchini.
Akizungumza
na viongozi wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) na Serikali jana jioni (Jumapili,
Januari 3, 2016) katika ukumbi uliopo Ikulu ndogo Songea, Waziri Mkuu ameutaka
uongozi wa mkoa kuhakikisha kuna
upatikanaji wa masoko kwa mazao mbalimbali pamoja na kuendelea kutoa
msukumo kwa wananchi.
Pia,
ameupongeza uongozi wa mkoa huo kwa kutoa msukumo kwa wananchi na kufanyakazi,
na kusema ni jambo linalosaidia kupanda kwa pato la mtu mmoja mmoja, hata hivyo hakusita kuwashukuru kwa
mapokezi makubwa aliyopata.
“Nawapongeza
sana wana Ruvuma kwa kuongeza pato la ndani kutoka shilingi 654,227, hadi kufikia shilingi
1,800,000 kwa kipindi cha mika 4 tuendelee kujiweka vizuri kwa kuongeza pato la
mtu mmoja mmoja” alisema Waziri Mkuu.
Waziri Mkuu
Majaliwa pia amesisitiza kilimo cha
umwagiliaji katika maeneo yote yenye mabonde ili wakulima waweze kuvuna bila
kutegemea sana kipindi cha masika. Amesema ni lazima kuimarisha huduma muhimu
na kusisitiza matumizi mazuri ya fedha zinazopatikana katika mazao hayo.
Kwa upande
wake, Mkuu wa Mkoa wa Ruvuma, Said Thabit Mwambungu amesema zaidi ya asilimia 90 ya wananchi wa Ruvuma
hutegemea kilimo cha mazao mbalimbali ya
chakula na biashara yakiwemo mahindi,
mpunga ambao unalimwa sehemu za Tunduru na Songea vijijini, korosho ambazo zinalimwa sehemu za Tunduru, Namtumbo,
Nyasa, Mbinga na Songea vijijini na tumbaku
maeneo ya Namtumbo,Mbinga na Songea vijijini.
Alisema,
Ruvuma imekua ikizalisha chakula kwa kiwango cha utoshelezi na ziada kwa
kipindi cha mwaka 2012 - 2013, 2013 - 2014 hali hiyo imeendelea kuwa nzuri hadi
kipindi cha mwaka 2015 - 2016.
Mahitaji yakiwa ni tani 469,172 na ziada ikiwa
tani 1,950,111, ametaja baadhi ya sababu za ongezeko hilo la tani ni pamoja na matumizi ya dhana bora za kilimo, matumizi ya pembejeo za
kisasa na urahisi wa upatikanaji wa pembejeo, aliongeza Mkuu wa Mkoa.
Waziri Mkuu
Majaliwa ambaye jana (Jumapili, Januari 3, 2016) ameanza ziara ya kikazi ya
siku nne mkoani Ruvuma, leo siku ya
jumatatu atakuwa na shughuli za
kufungua tawi la Benki ya Posta mjini
Songea, kukagua maghala ya Wakala wa
Taifa wa Hifadhi ya chakula (NFRA) kanda ya Songea na kukagua Makao Makuu
ya Halmashauri ya Wilaya ya Songea.
Kupitia
ziara hii Serikali ina lengo la kuona hali halisi ya utendaji wa shughuli za
maendeleo kutoka kwa watendaji mbalimbali, kuwatia moyo na kuweka
msisitizo katika maeneo yaliyopewa
kipaumbele hasa katika sekta ya Afya.
IMETOLEWA
NA:
OFISI YA
WAZIRI MKUU,2 MTAA WA MAGOGONI,
S. L. P
3021,11410 -DAR ES SALAAM
JUMATATU,
JANUARI 4, 2016.
Papo kwa Papo >>>> Pata Picha, Habari za Siasa, Kijamii, Biashara, Muziki na Michezo na Nyingine kwa kujiunga na mimi hapa…..FACEBOOK , TWITTER , INSTAGRAM , Pia tutumie tukio la Picha kwa WhatsApp .
|
No comments:
Post a Comment