Ajali hiyo
ilitokea jana October 01,2015, jioni majira ya saa kumi na nusu katika kijiji
cha Kasaka eneo la mzani, wakati askari hao wakisafiri kutoka kikosini
Bulombora kwenda mjini Kigoma kikazi kwa kutumia gari lenye namba 57117 JW 09
mali ya jeshi, ambalo lilipasuka tairi zote za nyuma na kupoteza uelekeo.
Akiongea na
waombolezaji waliofika katika viwanja vya hospitali ya mkoa wa
kigoma(Maweni)kwaajili ya kuaga miili ya marehemu Mkuu wa vikosi vya Kigoma,
Kanali Msuya alisema jeshi limepoteza nguvu kazi ya Taifa .
Alisema
mpaka sasa taratibu zote za kusafirisha miili hiyo zimeshakamilika miili yote
itaondoka kwa usafiri wa magari hadi mwanza na kesho watasafirishwa na ndege ya
jeshi kwenda dar es salaam kwaajili ya kupelekwa kwenye mikoa yao kwa maziko.
Kanali msuya
aliwataja waliofariki katika ajali hiyo kuwa ni MT 54407 SGT Ally Kambangwa
mkazi wa mtwara,MT 108151 PTE Abeli Maisha mkazi morogoro,SM Eugini Bitati
mkazi wa kibondo.
Wengine ni
AH 7190 SM Saidi Sadara mkazi wa Shinyanga,RES Bakari Kibaya mkazi wa Tanga,RES
Fredrick Kahemela mkazi wa arusha.
Msuya
aliwataja majeruhi pia majina yao kuwa ni Benadicto Ndokeye,Raphael
Yohana,Athanas Emanuel,Abuu Nzoge,Abubakari peter,Abubakari Msubi na Denis
Manyanya.
Wengine ni
Edward Nyanda,Elias Magessa,Gofrey Maliki,King Kasefu,Kamilius Agida,Stive
Denis,Saidi Omary,Saidi Zuberi,Shabaani Zakari,victor John,Jackson Nyarubu na
Mohamed Nyimbo.
Askari
wengine 22 ambao wamejeruhiwa na kulazwa katika Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa
Kigoma, Maweni, kufuatia ajali hiyo, wametajwa kuwa ni Benedicto Ndokeye,
Raphael Kibamba, Antanas Emmanuel, Abuu Nzoghe Hassan, Abubakar Mathias Peter,
Bakari Sinuki Mwaisunga, Deus Manyanya Charles, Peter Edward Nyanda, Elias
Masaga Magesa, Geofrey Peter Malik na King Lucas Kasofu.
Wengine ni
Camilius William Hagida, Lameck John, Martin Andrew Lupatu, Steven Denis Mtege,
Said Omary Kitogo, Said Suleiman Zuberi, Shabani Idd Zakaria, Victor Adelbert,
Jackson John Nyarubi, Mohamed Jackson Nyimbo na Abubakar Hassan Mkubi, ambao
kulingana na Mganga Mfawidhi wa Hospitali hiyo Dr.Fadhil Kibaya wengi hali zao
zinaendelea vizuri. |
No comments:
Post a Comment