Mahakama ya
Hakimu Mfawidhi wa Wilaya ya Misungwi, mkoani Mwanza, imemhukumu msanii wa
ngoma za asili, Mng’ahwa Kazanza (42), kwenda jela miaka 10 kwa kosa la
kumiliki fisi wawili na kuwatumia kwenye sanaa zake bila kibali.
Awali
akisomewa mashtaka katika mahakama hiyo na Mwendesha Mashtaka wa Polisi, Doroth
Mgenyi, ilielezwa mahakamani hapo kuwa mnamo Septemba 28, mwaka huu, kwenye
Kijiji cha Sisu wilayani Misungwi, majira ya saa 7:30 mchana, Mng’ahwa Kazanza
(42) alikamatwa akiwa na fisi wawili wenye thamani ya Sh milioni 4.8.
Mara baada
ya kusomewa mashtaka, msanii huyo alikiri kosa hilo na kudai alikuwa akiwatumia
fisi hao katika sanaa zake bila kutambua kama ni kosa kuburudisha mashabiki
wake kwa lengo la kuongeza kipato.
Kutokana na
kukiri huko, Hakimu Mfawidhi wa Mahakama hiyo, Ruth Mkisi, ilimtia hatiani kwa
kosa la kupatikana na nyara za Serikali kinyume cha sheria Na. 5 ya mwaka 2009
na kumhukumu kwenda jela miaka 10 au kulipa faini ya Sh 4,840,000 ili iwe
fundisho kwa watu wengine wanaomiliki nyara za Serikali kinyume cha sheria.
Msanii huyo
alishindwa kulipa faini hiyo na hivyo kwenda jela kutumikia adhabu hiyo ya
miaka 10.
Chanzo:
Mtanzania
Papo kwa Papo >>>> Pata Picha, Habari za Siasa, Kijamii, Biashara, Muziki na Michezo na Nyingine kwa kujiunga na mimi hapa…..FACEBOOK , TWITTER , INSTAGRAM , Pia tutumie tukio la Picha kwa WhatsApp +255789925630.
|
Tuesday, October 06, 2015
SHERIA YETU:-Msanii jela miaka 10 kwa kumiliki fisi.
Tags
# HABARI
Sambaza Hii
Chief Editor | Mhariri
HABARI
Labels:
HABARI
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
Kuhusu Mwandishi
Journalist / Chief Editor / Tanzanian Blogger
Simu: 0756830214 / 0620197747 / 0789925630.
No comments:
Post a Comment