![]() |
Mwenge.......chomaaa......chomaaaa........ Makabidhiano ya Mwenge wa Uhuru 2013 kati ya Mkoa wa kagera na Kigoma (Julai
09,2013) kwenye Mpaka wa Wilaya ya
Biharamulo na Kakonko.
|
Mbio za Mwenge
wa Uhuru zilizoanza Mkoani Kagera (Julai 01,2013) zimehitimishwa (Julai
09,2013) katika wilaya ya Biharamulo na
kukabidhiwa Mkoani Kigoma kupitia wilaya ya Kakonko .
Mkuu wa Mkoa
wa Kagera Kanali Mstaafu Fabian Masawe akikabidhi Mwenge huo (Julai 09,2013) kwa Mkuu wa Mkoa wa Kigoma Kanali Mstaafu Issa
Machibya, amesema Mwenge huo ukiwa Mkoani Kagera umepitia miradi 78 ya Maendeleo ya Wananchi iliyogharimu jumla ya
Shilingi Bilioni 11.5 ,ikiwa ni Fedha zitokanazo na Nguvu za Wananchi,Serikali Kuu,Halmashauri na Wahisani.
Kwa upande
wake Mkuu wa Mkoa wa Kigoma Luteni Kanali mstaafu Issa Machibya alisema Jumla ya miradi 64 yenye thamani ya Shilingi
Bilioni 13.7 itapitiwa na Mbio hizo za Mwenge wa Uhuru kwa Mwaka huu 2013 kwa kukimbizwa Wilaya
Saba za Mkoa huo ambapo ukihitimisha mbio zake(Julai 16,2013) utakabidhiwa Mkoani Katavi.
Akiwaaga
Viongozi wa Mkoa wa Kagera na kuingia Mkoani Kigoma ,Kiongozi wa mbio za Mwenge
Kitaifa mwaka huu 2013, Bw Juma Ally Sumai alisema kuwa amefurahishwa na
mshikamano pamoja na Ushirikiano uliopo kwa viongozi na watendaji mkoani Kagera katika kusimamia na kuleta maendeleo kwa
wananchi.
Aidha Mwenge wa uhuru uliwashwa (May 06,2013) mjini Pemba katika Kijiji
cha Chokocho na Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dr. Ali Mohamed Shein na unatarajiwa
kuhitimisha mbio zake Mkoani Iringa october
14,2013.
Kauli mbiu ya Mwaka huu 2013 katika Mbio hizo za Mwenge wa Uhuru ni''Watanzania
ni wamoja''Tusigawanywe kwa Misingi ya tofauti zetu za Dini,Itikadi,rangi na
Rasilimali''
This year’s
race also coincide with the ”50th anniversary of Zanzibar’s
Revolution.Other message to be promoted during the race included;” Fight
against HIV/AIDS and drugs use” and “Fight against corruption” The Uhuru Torch
is one of Tanzania’s national symbols.It symbolizes freedom and
hope.
No comments:
Post a Comment