Tangu Waziri
wa Haki wa Swaziland, Ndumiso Mamba, anaswe kitandani anavunja amri ya sita na
mke wa Mfalme wa nchi hiyo, Makhosetive Dlamini ‘Mfalme Mswati III’, hali ni
mbaya kwa wake wa kiongozi huyo.
Mamba,
alinaswa kwenye kitanda cha mke wa 13 wa mfalme huyo, Nothando Dube na tangu
wakati huo, walinzi wa Mfalme Mswati, wamepewa madaraka makubwa ikiwemo
kuwacharaza bakora hata barabarani na mbele za watu.
Inaelezwa
kwamba wake wa Mfalme Mswati wanafungiwa ndani kama kuku, inapotokea wanakwenda
sehemu wanakuwa chini ya ulinzi mkali.
Ripoti
zinasema kuwa endapo barabarani mke wa mfalme atachepuka kwenda hata msalani
bila taarifa au atasalimiana na mtu ambaye walinzi wanamjua, hata kama ni ndugu
yake, mwanamke husika hucharazwa bakora kama ng’ombe.
“Ukiwa mke
wa Mfalme Mswati ni mateso makubwa. Unavyoishi haina tofauti na ng’ombe
anavyochungwa. Ukiwa unatembea barabarani unatakiwa ufuate uelekeo anaotaka
bodigadi, ukikosea kidogo unachapwa bakora na virungu.
“Mambo yalikuwa mabaya lakini sasa ni mabaya
mno. Kwa sasa nataka kutoka lakini mfalme hataki kuruhusu niondoke. Nipo kama
mfungwa, saa 24 nachungwa, sina uhuru hata kidogo,” alisema Nothando.
Mfalme
Mswati III akiwa na baadhi ya wake zake.
|
Mwanaharakati
wa demokrasia anayepingana na mtindo wa maisha ya Mfalme Mswati, Lucky Lukhele,
aliwahi kuwaambia waandishi wa habari kwamba siyo Nothando tu, wake wote wa
kiongozi huyo wanaishi katika mazingira magumu afadhari ya wafungwa.
“Kuna mke
mmoja wa mfalme alikutwa getini na walinzi, tena getini kwenyewe kwa ndani
halafu geti lilikuwa limefungwa na funguo wanazo walinzi. Ajabu ni kwamba
walinzi walipomkuta pale hawakuuliza mara mbili, walimpiga na kumuumiza mno,”
alisema Lukhele bila kutaja jina la mke huyo wa mfalme.
Kwa upande
mwingine, inaelezwa kuwa mtindo wa maisha ya Mfalme Mswati na wakeze,
umesababisha mpaka sasa akimbiwe na wanawake watatu.
Mke wa sita
wa mfalme huyo, Angela “LaGija” Dlamini, ndiye anatajwa kuwa mwanamke wa hivi
karibuni zaidi kuondoka katika himaya ya mfalme huyo.
Mke wa 12 wa
mfalme, Inkhosikati LaDube, alitimuliwa Desemba mwaka jana kwa kile
kilichobainishwa kwamba aligombana na bodigadi wake.
Taasisi ya
Swaziland Solidarity Network ilieleza kwamba Dlamini, alikimbia makazi ya
mfalme baada ya kuwa kwenye mateso kwa miaka kadhaa.
Dlamini,
aliaga anakwenda kuwasalimia wazazi wake kwenye Mji wa Hhohho, lakini
aliporuhusiwa alitimka jumla.
Mfalme
Mswati pamoja na tabia ya kupenda kuoa mabikra, vilevile anatuhumiwa kujilimbikizia
utajiri wa kutisha, hivi karibuni Jarida la Forbes lilimtaja kwamba anamiliki
utajiri wenye thamani ya zaidi ya dola milioni 200 (shilingi bilioni 300).
Imeandikwa
na globalpublishers.
No comments:
Post a Comment