Wanawake Wajawazito wametakiwa kufika mapema katika Vituo vya Afya,
Zahanati na Hospitali hasa wanapokaribia kujifungua ili
kuepuka kujifungulia njiani. 
  
Hayo yamesemwa  na muuguzi wa kituo cha afya Bunazi  Bi Blandina  Bahati  muda
mfupi baada ya kumpokea  mwanamke mmoja  mkazi wa kijiji cha 
Ibanga  kata ya Nsunga  wilayani  Missenyi  mkoani Kagera
ambaye amejifungulia njiani wakati  akitembea  kwa mguu 
kuelekea  kituoni hapo. 
 
Bi  Lethicia  Didas  akiongea na Radio Kwizera  mara baada ya
kufika  kituoni hapo kupatiwa huduma   amesema  alipata
uchungu  kabla  hajafika kituoni ndipo akalazimika  kujifungulia kwenye shamba la miwa  bila
kuwa na msaada kutoka kwa wataalam tofauti na ndugu  yake aliyekuwa
anamsindikiza.     
 
Nae Bi Peace  Elnest aliemsindika mama
huyo amesema  chanzo  cha kujifungulia njiani  ni ukosefu wa
fedha  ya nauli   ambapo  kutoka nyumbani  hadi 
kufika  kituo cha afya  Bunazi ni umbali wa kilometa 15 na 
usafiri wa pikipiki unagharimu  kiasi cha shilingi  elfu tano. 
  
 
 | 
No comments:
Post a Comment