Wilaya ya Ngara na Changamoto ya Kuhifadhi Vyanzo vya Maji. - Mwana Wa Makonda

Muhtasari

X-BET


Post Top Ad

Wednesday, June 06, 2018

Wilaya ya Ngara na Changamoto ya Kuhifadhi Vyanzo vya Maji.

Wananchi Wilayani Ngara Mkoani Kagera wanahimizwa kupitia Siku ya Mazingira Duniani June 5, kushirikiana na Serikali pamoja na Wadau kuhakikisha vyanzo vya maji vinalindwa ipasavyo ili view endelevu sambamba na  kupanda miti na maua ili kuweka mazingira safi na salama.

 Bw Moris Mombia  ni Afisa Tarafa wa Rulenge kwa Niaba ya Mkuu wa wilaya ya Ngara Luteni Kanal Michael Mtenjele katika kilele cha maadhimisho ya siku ya mazingira duniani, yaliyofanyika kiwilaya kwenye mamlaka ya mji mdogo wa Rulenge amehimiza kuweka msukumo wa pamoja katika kuhamasisha Jamii, kuhifadha na kutunza mazingira ili kudhibiti uhalibifu mkubwa wa mazingira unaopelekea mabadiliko ya tabia nchi.
Nae Afisa Usafi na Mazingira Wilayani Ngara Bw. Waziri Nicholaus amesema elimu imetolewa kwa wadau wa mazingira waweze kuhamasisha jamii kutunza na kusafisha mazingira huku akisisitiza matumizi ya nishati mbadala kwa lengo la kupunguza matumizi makubwa ya mkaa yanayosabisha uharibifu wa mazingira

Maadhimisho ya Siku ya Mazingira Duniani hufanyika Juni 05 kila mwaka ambapo kwa mwaka huu imeadhimishwa chini ya kauli mbiu inasemayo MKAA NI GHARAMA TUTUMIE NISHATI MBADALA.
 
 
 
 
 
 

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad