![]() |
Mfuko
unaosadikiwa kuwemo Kitoto Kichanga.
Mtoto
mchanga anaekadiriwa kuwa na umri wa miezi sita amekutwa ametupwa akiwa tayari
amefariki kwenye mfuko wa kubebea nguo leo June 5, 2018 katika Kijiji
cha Muweza,Kata ya Mabawe Wilayani Ngara Mkoanai Kagera.
Akizungumza
na Radio Kwizera FM, Mtendaji wa Kata
ya Mabawe Bw Jonas Gwassa amesema amepokea
taarifa za tukio hilo kutoka kwa raia wema ambapo baada ya kufika eneo la tukio
amekuta mfuko huo na alipo ufungua akaona mtoto huyo akiwa amefariki.
![]() |
![]() |
Bw.Gwassa ameeleza kwamba ametoa taarifa Kituo
Kidogo cha Polisi Kabanga lakini mpaka Radio Kwizera inaondoka katika eneo la
tukio walikuwa hawajafika.
Baadhi ya Wananchi
waliofika katika eneo hilo wamelaani kitendo hicho na kuwa ni kitendo cha
kinyama huku wakiwataka vyombo vya usalama kumchukulia hatua kali za kisheria
mtu yeyote atakaye bainika kuwa amefanya tendo hilo.
Hata hivyo
jeshi la polisi Wilayani Ngara limethibitisha kutokea kwa tukio hilo na uchunguzi
unaenedelea kubaini muhusika wake.
|

No comments:
Post a Comment