Taswira ya Ubunifu wa Mwanafunzi huyu Shule ya Msingi Kaniha,Biharamulo,Kagera. - Mwana Wa Makonda

Muhtasari

X-BET


Post Top Ad

Thursday, June 14, 2018

Taswira ya Ubunifu wa Mwanafunzi huyu Shule ya Msingi Kaniha,Biharamulo,Kagera.

 Mwanafunzi wa shule ya msingi Kaniha wilaya ya Biharamulo mkoani Kagera Masembo Sizya wa darasa la nne ametumia ubunifu wa kiakili na kuunda mashine ya kusaga akitumia vifaa vya plastiki akiongeza nyaya za umeme na mota ya radio.

 Mwanafunzi huyo pia ameunda gari linalotembea bila mafuta ispokuwa nishati ya umeme akionesha jinsi vijana wanavyoweza kujikita katika ufundi wakiwezeshwa kupata vitendea kazi.

Alikuwa katika maonesho ya wiki ya elimu kata ya Nyantakara wilayani Biharamulo mkoani Kagera,yaliyofanyika kiwilaya na kuwashangaza wadau mbalimbali waliokuwa katika maonesho hayo na kudai serikali haina bidi kuandaa shule zenue watoto walio na vipaji maalum.
Watoto wengine walionesha umahili katika kuchonga , kuchora kufinyanga na kiuunda maumbile ya sura ya nchi kupitia masomo ya stadi za kazi, jografia na saynsi "Mwanzoni waliniita mwizi au taahila kwa kubeba na kukusanya makopo au chupa za plastiki lakini sikukata tamaa naongeza ujuzi" Alisema mwanafunzi huyo.

 Hata hivyo Kaimu Afisa elimu idara ya msingi wilayani Biharamulo Amosi Nyamtera amesema ili kuibua vipaji ngazi za vijiji na hata mjini no kuwaibua watoto wengine wenya ulemavi kufundishia na kukuza vipaji vyao.

Na-Shaaban Ndyamukama. 

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad