
Na Shaaban
Ndyamukama-Radio Kwizera Ngara.
Bodi ya Wakulima Kahawa ya chama cha wakulima cha Ngara
Farmers mkoani Kagera iliyomaliza muda wake imeshindwa kukabidhi mali za chama
hicho kwa wajumbe wa bodi mpya
ambayo imeundwa mwaka huu (2018) baada
ya kuwepo mgogoro wa nyaraka na mali inayokabidhiwa.
Akitoa
taarifa ya Mali za aina mbalimbali za Ngara Farmers aliyekuwa Mwenyekiti wa
bodi ya zamani Bw.Steven Runzanga
amesema wajumbe wa bodi mpya wapokee
majengo, mitambo, na nyaraka yakiwemo madeni ya makarani, na deni la benki ya
NMB la Shilingi milioni 50.7.

Bw.Runzanga amesema katika chama hicho
kumeshindikana ulipaji wa madeni kutokana na kushindwa kuuza wala kununua
kahawa kutoka kwa wakulima zaidi ya miaka mitatu iliyopita baada ya kukabidhiwa
chama kisichokuwa na fedha kama mtaji wa
uzalishaji.
Aidha Bw.Runzanga amesema bodi ijipange kuboresha miundombinu ya kiwanda cha
kukoboa kahawa badala ya kupeleka kwenye viwanda vingine na kuongeza gharama za
uendeshaji na lakini pia kumpunja mkulima pamoja na kupunguza uaminifu katika
ushindani wa kibiashara.
Baadhi ya
wajumbe wa bodi mpya ya mpito kwa kipindi cha mwaka mmoja wamehoji mali
iliyo halisi ya kuonekana au nyaraka mbalimbali ambazo hazifafanui
uhalisia na kuondoa wasiwasi katika kutekeleza majukumu.

Hata hivyo
Mwenyekiti mpya wa bodi ya chama hicho Bw
David Bukozo (Pichani ) amesema wajumbe wenzake hawawezi kukabidhiana mali za chama
cha wakulima hadi kufanya marekebisho ya nyaraka na takwimu za mali baada ya
kubainika baadhi kuwa na utata katika umiliki wake.
Bw.Bukozo pia amekanusha bei ya kahawa inayotangazwa ya
Shilingi 1000 na Shilingi 1200 kwa kilo sababu serikali haijatangaza ispokuwa kiwango hicho
ni sehemu ya mauzo kwenye chama cha ushirika hivyo wakulima wajipange kuuza
kahawa yao mnadani katika soko la Moshi.

Amewataka
wakulima wa zao hilo kuanza uvunaji na kulipeleka kwenye chama cha ushirika cha
Ngara Farmers na mkulima hatapewa fedha taslimu bali atafungua akaunti yake
binafsi katika taasisi za kibenki kwa
watakaokuwa na a kiwango kikubwa cha mauzo.
Amesema kwa
mkulima mwenye kuuza kahawa kuanzia zia kilo moja kufikia tani moja atafungua
akauti kwa kutumia simu yake ya mkononi
akitumia mtandao wa mawasiliano na kuingiziwa malipo kwa lengo la kudhibiti
matukio ya usalama .
Aidha Meneja
wa Chama hicho Bw Hamphrey Kachecheba
amesema baada ya kupata akaunti kutajazwa fomu maalum za usajili kutoka taasisi
za kibenki kwa ajili ya kuwabaini wasiojua kusoma na kuandika kuchagua watu
waaminifu wa kuwachukulia fedha za malipo ya mauzo.
No comments:
Post a Comment