Zahanati Nne
katika Tarafa ya Rulenge na Murusagamba Wilayani Ngara Mkoani Kagera zimepokea
msaada wa dawa zenye thamani ya Shilingi milioni 15.4 kutoka kwa Kampuni ya
kabanga Nickel wilaya humo.
Afisa Mahusiano
wa Kampuni hiyo Bw.Francis Wikedzi
amesema dawa hizo zitatumika kutibu magonjwa mbalimbali katika zahanati za
Mumiramila, Bugarama, Muganza na Mukubu ili wananchi wapate hududma nzuri
za matibabu.
Bw Wikedzi amesema kampuni hiyo inahitaji
kusaidiana na serikali ya wilaya na vijiji kusaidia kupunguza changamoto
zilizopo katika kijamii.
Katibu Tawala
wa wilaya ya Ngara Bw Vedastus Tibaijuka
ameishukuru kampuni hiyo kwa msaada wake na kwamba kampuni inashiriki
kuboresha miundombinu katika sekta ya elimu na Afya ili kuharakisha maendeleo
ya wilaya.
Na-Radio Kwizera.
|
Tuesday, May 29, 2018
Dawa za Binadamu zatolewa kwa Zahanati Nne wilayani Ngara na Kampuni ya Kabanga Nickel.
Tags
# HABARI
Sambaza Hii
Chief Editor | Mhariri
HABARI
Labels:
HABARI
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
Kuhusu Mwandishi
Journalist / Chief Editor / Tanzanian Blogger
Simu: 0756830214 / 0620197747 / 0789925630.





No comments:
Post a Comment