Picha/ Habari -Idadi ya Vifo yaongezeka Ajali ya Wakimbizi Ngara,Kagera. - Mwana Wa Makonda

Muhtasari

X-BET


Post Top Ad

Saturday, March 31, 2018

Picha/ Habari -Idadi ya Vifo yaongezeka Ajali ya Wakimbizi Ngara,Kagera.


Baadhi ya wagonjwa wakiandaliwa kwa safari ya  Bugando Mwanza eneo la Uwanja wa ndege Ruganzo,wilayani  Ngara mkoani Kagera.
Basi hilo Eneo la Ajali.

 Ajali hiyo imetokea saa 10 jioni  katika mteremko  wenye kona kali wa mlima K9 barabara kuu ya Benaco –Ngara  ambapo Basi lilipoteza mfumo wa breki lenye namba za usajili T 331 DFV aina ya YUTONG Mali ya kampuni ya Lugano (Kampuni ya Mtipa Investment ) ya mkoani Kigoma liligonga Basi T 765 DLD aina ya TATA ambapo lilipoteza uelekeo na kusababisha Vifo na Wengine Kujeruhiwa.
Afisa mwandamizi wa Shirika la kuhudumia wakimbizi UNHCR wilayani Ngara Bi. Irene Babu.

Idadi ya vifo vya Wakimbizi waliopata ajali kwenye mteremko wenye kona kali wa K9 katika kijiji Kasharazi wilayani Ngara mkoani Kagera, imeongezeka na kufikia 8 baada ya wawili kufariki wakipatiwa matibabu katika Hospitali ya Murugwanza na mmoja katika hospitali ya Nyamiaga.

Afisa Mwandamizi wa Shirika la kuhudumia Wakimbizi UNHCR wilayani Ngara Bi. Irene Babu amesema kati ya hao Nane waliopoteza maisha, Sita ni Wakimbizi na Watanzania ni wawili ambapo kati ya hao Watanzania, mmoja mkazi wa Kasharazi aliyekuwa akiendesha baiskeli ambaye basi lilimwangukia na mwingine alikuwa Mfanyakazi wa Shirika la Kimataifa la Uhamiaji (IOM).
Majeruhi wote waliopata rufaa wamekwishasafirishwa kwa ndege ya UNHCR kwenda hospitali ya Bugando kupitia uwanja wa ndege wa Ruganzo uliopo wilayani Ngara
Mganga Mkuu wa Hospitali ya Murugwanza ya Wilayani Ngara Dr. Remmy Andrew amesema katika Hospitali hiyo alipokea Majeruhi 65 kati yao 30 ni Wanawake na 35 ni Wanaume  na kwamba waliotibiwa na kuruhusiwa ni 40 na waliopatiwa rufaa kwenda Hospitali ya Bugando ni 7

Aidha Mganga Mfawidhi wa Hospitali ya Nyamiaga Dr. Simon Kyamwenge amesema Hospitali hiyo ilipokea Majeruhi 31 kati yao Wanaume ni 24 na Wanawake 7 na kwamba mpaka sasa ameruhusiwa mtu mmoja pekee.

Pia Dr. Kyamwenge amesema Majeruhi 12 wenye hali mbaya wamepewa rufaa ya kupelekwa katika Hospitali ya Bugando Jijini Mwanza kwa matibabu zaidi.


Habari/Picha kwa Hisani ya RADIOKWIZERA.CO.TZ

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad