Pichani Basi hilo likiwa limeharibika Vibaya.
Ajali hiyo
imetokea saa 10 jioni katika mteremko wenye kona kali wa mlima K9 barabara kuu ya
Benaco –Ngara ambapo Basi lilipoteza
mfumo wa breki aina ya Higer lenye namba za usajili T 331 DFV ambalo lililigonga
kwa nyuma Basi linguine aina ya TATA Star lenye namba za usajiri T 765 DLD Mali
ya kampuni ya Lugano (Kampuni ya
Mtipa Investment ) ya mkoani Kigoma na kusababisha Vifo vya Watu watano papo
hapo na wengine wengi kujeruhiwa.
|
![]() |
Wananchi wakiendelea kutoa msaada wa
kukata miti ili kuokoa Majeruhi .
|
![]() |
Kamanda wa
Polisi Mkoa wa Kagera, Agustino Olomi akizungumzia ajali hiyo amesema miili ya
waliofariki dunia bado haijatambuliwa pamoja na idadi ya majeruhi.
Amesema
waliofariki dunia ni Wanawake watatu na Wanaume wawili ambapo Kati yao yupo mkazi wa
Kasharazi aliyekuwa akiendesha baiskeli ambaye basi lilimwangukia.
|



![]() |
Mmoja wa
mashuhuda Bw. Amiri Salum ambaye ni Dereva aliyekuwa nyuma ya mabasi hayo
akitokea Biharamulo, amesema wakati magari yakimalizia mteremko ndipo ajali
ilipotokea ambapo yote yalielekea kwenye mashamba ya wakulima
Aidha majeruhi wa ajali hiyo wamekimbizwa kwenye hospitali za Murugwanza na Nyamiaga za wilaya ya Ngara kwa ajili ya matibabu zaidi.
Habari/Picha kwa Hisani ya RADIOKWIZERA.CO.TZ
|




No comments:
Post a Comment