
![]() |
“Madarasa
haya yalijengwa mwaka 1953 yalikuwa imara kuta zake lakini kutokana na kujengwa
mlimani uliibuka upepo na kuezua paa na
kusababisha wanafunzi na walimu kukimbilia majengo mengine” Alisema Sayi
Amesema
tangu kuezuliwa kwa vyumba viwili na ofisi ya walimu umekuwa na usumbufu wa walimu kusongamana kwenye chumba cha maktaba na veranda na kusahihisha
madaftari ya wanafunzihali ambayo inakatisha tamaa kazi ya ualimu.
|

![]() |
Mahitaji mengine
ni uhaba wa matundu ya vyoo, yanahitajika 13 upungufu matundu sita na
nyumba nane kati ya 12 zinazohitajika ambapo alishauri serikali ya kijiji na
halmashauri kuboresha miundombinu ya shule hiyo.
Katika hatua
nyingine wanafunzi wa shule hiyo
wameiomba serikali kuwapatia mwalimu wa kike
wakuweza kusikiliza changamoto zao za kimaumbile kwani wanakuwa na aibu
kuzieleza wazi mbele ya walimu wa kiume.
Wanafunzi na
walimu wa kiume walisema aliwahi kuletwa mwalimu wa kike shule ya msingi Rwimbogo lakini kutokana na
kuwepo matukio ya ujambazi na watu kuuawa na wengine kujeruhiwa mwalimu huyo
alihamia sehemu nyingine.
Mmoja wa
walimu wa Shule hiyo Andrea Gabriel aliyekuwa akisahihisha madaftari ya wanafunzi kwenye veranda ya
chumba cha maktaba, aliomba serikali kujenga ofisi ya walimu kuepukana na
usumbufu wa mvua kulowanisha madaftari
|
![]() |
Mwenyekiti
wa Serikali ya Kijiji cha Mukalinzi,Bw.Richard Magogolo amesema wananchi wameanza
kuchangia Sh 2000 kila Kaya kukarabati vyumba hivyo ingawa michango
inasuasua kutokana na maagizo ya
serikali ya kuifuta.
Amesema
mkakati mkubwa wa wananchi ulikuwa ni kujenga kituo cha polisi kuimarisha
ulinzi na usalama ambapo kituo hicho kimefikia hatua ya renta kwa thamani ya
Sh8 milioni na malengo hadi kukamilika
kitagharimu Sh15 milioni
Akizungumza
katika kikao cha Walimu Wakuu, Maafisa Elimu Kata na Watendaji wa Kata hivi karibuni, Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya wilaya ya Ngara, Bw. Aidan Bahama
amesema iwapo wananchi wataanzisha miradi kwa kuweka vifaa vinavyopatikana
kwenye mazingira yao serikali itapeleka
fedha kuwaunga mkono
|

No comments:
Post a Comment