Matokeo ya Taifa ya Kidato cha Nne 2017 -Ingia Hapa Kuyapakua Yote. - Mwana Wa Makonda

Muhtasari

X-BET


Post Top Ad

Wednesday, January 31, 2018

Matokeo ya Taifa ya Kidato cha Nne 2017 -Ingia Hapa Kuyapakua Yote.

Baraza la Mitihani la Taifa (Necta) limetangaza matokeo ya kidato nne ambapo ufaulu umeongezeka kwa asilimia 7.

Jumla ya watahiniwa  385, 767 walisailiwa kufanya mtihani kidato cha nne mwaka 2017, kati yao 287,713 sawa na asilimia 77.09 ndio wamefaulu ambapo wasichana ni  143,728 sawa na asilimia 75.21 na wavulana 143,985 sawa na asilimia 79.06.

Akitangaza matokeo hayo leo Januari 30, 2018 Katibu Mtendaji wa Necta,  Dk Charles Msonde amesema mwaka 2016 watahiniwa waliofaulu walikuwa 277,283 sawa na asilimia 70.09.

Amesema matokeo ya watahiniwa 50 wa shule ambao walipata matatizo ya kiafya na kushindwa kufanya baadhi ya masomo ya mitihani hiyo, watapata fursa hiyo mwaka huu,2018.

BOFYA HAPA CHINI KUYATAZAMA MATOKEO YOTE.
 

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad