Kiwango Kizuri mechi na Singida United champa zawadi ya gari Said Hamis Ndemla. - Mwana Wa Makonda

Muhtasari

X-BET


Post Top Ad

Friday, January 19, 2018

Kiwango Kizuri mechi na Singida United champa zawadi ya gari Said Hamis Ndemla.

Simba SC imeshinda kwa mabao 4-0 dhidi ya Singida United katika mechi hiyo ilikuwa inasubiriwa kwa hamu kubwa na mashabiki wa soka nchini.
Mchezaji Said Hamis Ndemla alitengeneza mabao mawili moja akifunga Emmanuel Okwi na jingine Asante Kwasi.

Mwenyekiti wa Kamtai ya Usajili ya Simba, Zacharia Hans Poppe ametoa zawadi ya gari kwa mchezaji huyo wa Simba SC, Said Hamis Ndemla.

Hans Poppe ametangza kumpa Ndemla gari baada ya kuonyesha kiwango kizuri cha kuvutia katika mechi dhidi ya Singida United, Jana January 18,2018.

 “Nilikuwa nikimfuatilia kama ambavyo nimekuwa nikisema nahitaji mchezaji mwenye nidhamu na ambaye hawezi kubadilika. Utaona Ndemla amekuwa benchi lakini akiingia uwanjani anaonyesha mchango wake,” alisema.

“Tena pamoja na kukaa benchi, hakuwahi kuonyesha utovu wa nidhamu. Badala yake kila akipata nafasi amekuwa akijituma na kuisaidia timu.”

Hii ni mara ya pili Hans Poppe anatoa gari kwa mchezaji wa Simba SC. Alianza na Hussein Zimbwe aliyempa gari aina ya Toyota Raum. Lakini akaonyesha gari aina ya Toyota Lactic na kusema atapewa mchezaji atakayefanya vizuri.

Kuhusiana na aina, leo amesema: “Aina utaijua baadaye ila gari haiko mbali. Hivyo tutaangalia siku yenye nafasi atakabidhiwa.”

MSIMAMO WA LIGI ULIVYOSASA.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad