Zaidi ya Watu 50 wakamatwa na Jeshi la Polisi Kigoma kwa tuhuma za Mauaji na kuharibu Mali kwa kuchoma Moto kijiji cha Kabanga. - Mwana Wa Makonda

Muhtasari

X-BET


Post Top Ad

Tuesday, September 05, 2017

Zaidi ya Watu 50 wakamatwa na Jeshi la Polisi Kigoma kwa tuhuma za Mauaji na kuharibu Mali kwa kuchoma Moto kijiji cha Kabanga.

Pichani ni Mali mbalimbali zilizoteketezwa kwa Moto na Baadhi ya Wananchi katika kijiji cha Kabanga wilayani Kasulu mkoani Kgoma.

Mtu mmoja anayejulikana kwa jina la Emmanuel Songoye ameuawa kwa kuchomwa moto na Wananchi katika kijiji cha Kabanga wilayani Kasulu mkoani Kigoma katika tukio ambalo pia wameteketeza kwa moto nyumba saba, magari mawili, pikipiki nne na mali za familia za watu sita ambao wanawatuhumu kufanya mauaji ya watu kijijini hapo kwa njia mbalimbali ikiwa ni pamoja na ushirikina ili watajirike.


Kamanda wa Polisi mkoa wa Kigoma Naibu Kamishna wa Polisi Ferdinand Mtui amesema zaidi ya watu hamsini wamekamatwa kuhusiana na tukio hilo lililotokea Jana September 4,2017 huku Kaimu mkuu wa wilaya ya Kasulu Kanali Marco Gaguti ambaye pia ni mkuu wa wilaya ya Buhigwe akitoa wito kwa wananchi kuacha kujichukulia sheria mkononi.


No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad