Duru la tatu
la Ligi kuu ya Vodacom Tanzania Bara 2017/2018 Inatarajiwa kuendelea tena Leo
tarehe 15/9/2017 kwa wapenzi wa soka kushuhudia mchezo mmoja kuchezwa katika dimba la
Azam Complex Chamazi majira ya saa moja jioni kwa mujibu wa ratiba wakati Azam
FC itakapo wakaribisha Kagera Sugar.
Michezo
mingine ya Ligi Kuu inatarajiwa kuendelea tena hapo kesho tarehe 16 ambapo timu
tano zikitarajia kuingia katika viwanja mbali mbali, Majimaji FC ikiwakaribisha
mabingwa wa tetezi Yanga SC, Mtibwa Sugar ikicheza na Mbao FC,Tanzania Prisons
ikikabiliana na wanakuchele Ndanda FC, Lipuli FC dhidi ya Ruvu Shooting huku
Stand United chama la wana ikipepetana na Singida United.
Na hapo
keshokutwa tarehe 17 timu ya Mbeya City ikiwa na kibarua kizito kwa kuingia
uwanjani bila kocha wao, Kinnah F. Phiri waliyemtimua kufuatia matokeo mabovu
wanayoyapata itakabiliana na Njombe Mji katika mchezo wa namba 23 utakao pigwa
katikia dimba la Sokoine Jijini Mbeya ilhali Simba SC ikiwakaribisha Mwadui FC
katika dimba la uwanja wa Uhuru.
|
No comments:
Post a Comment