![]() |
|
“Kwa dhati
kabisa tunampongeza mwanachama wetu na mbunge wa Jimbo la Mpendae, kwa
kuonyesha utu na kuweka kando itikadi za kivyama kumsaidia Mbunge wa Singida
Mashariki, Tundu Lissu,” amesema Polepole kupitia taarifa hiyo.
Hata hivyo,
Polepole ameongeza kuwa wameamua kumpongeza mbunge huyo kwa kuonyesha uzalendo
wa hali ya juu, kwani katika matatizo ni vyema itikadi za kisiasa zikawekwa
pembeni ili kuweza kutatua kile ambacho kinakuwa kinawakabili.
Aidha Chama cha
Mapinduzi(CCM), kuwa wanachama wake na viongozi wa chama hicho wanaendelea
kumuombea apone haraka huku ikiitaka Serikali kuwatia nguvuni na kuwachukulia
hatua wote waliohusika na tukio la Mbunge wa Singida Mashariki, Tundu Lissu
aliyejeruhiwa na risasi Septemba 7,2017 kwa kupigwa risasi eneo la ‘area D’ mjini
Dodoma na watu wasiojulikana.
|








No comments:
Post a Comment