Vituo
vingine ni Mlimani Television, Tanga City Council Television, Imaan Television,
Morning Star TV, Africa Internet Television Ltd, Uhai Television Limited,
Barmedas TV, Target Television, Tabibu Television, Africa Swahili Television,
Cable and Satellite Consultancy Limited, WRM Television Network, Dira
Television, Parliament Media Trust (Bunge TV), Mahaasin Television.
Aidha
alifafanua kuwa Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania(TCRA) ndio yenye dhamana ya
kutoa leseni ya maudhui ya utangazaji wa Televisheni za aina mbili ambazo ni
Leseni za maudhui yanayotazamwa bila kulipia na maudhui ya Kulipia. Alizidi
kueleza kuwa leseni hizo zimegawanywa kimasoko ambapo kuna leseni za Kitaifa
ambazo zinapaswa kuonekana nchi nzima na leseni za Kimkoa ambazo huruhusiwa
kutangaza mikoa 10 ya Tanzania Bara, na leseni za kiwilaya ambazo huonekana
Mkoa mmoja.
Mgawanyo huu
wa kimasoko unatoa fursa kwa waombaji kutangaza maeneo wanayochagua kutokana na
uwezo wao wa kifedha na kiundeshaji ambapo maudhui hayo ya bila kulipia
yanapaswa kuonekana kupitia visimbuzi vya Makampuni ya Agape Associates
Limited, Basic Transmission Limited na Star Media (Tanzania) Limited. Visimbuzi
hivyo ni TING, STARTIMES, DIGITEK na CONTINENTAL.
Naibu Waziri
Wambura amevitaja vituo vyenye leseni ya soko la Kitaifa kuwa ni TBC1, Channel
Ten, East Africa Televisheni, Independent Televisheni, Star Televisheni, Clouds
TV na Bunge TV wakati vituo vyenye soko la kimkoa ni TV Imaan, Agape TV (ATV)
na TV1 na vituo vilivyobaki vina soko la kiwilaya.
Aidha, Kituo
cha TBC1 ambacho ni kituo cha Umma kinapatikana bila malipo ya mwezi kwenye
ving’amuzi vyote vya miundombinu iliyosimikwa ardhini na vile vinavyotumia
mitambo ya satelaiti kama vile Azam TV, DSTV na Zuku. Kituo cha TBC 1
kinalazimika kuonekana bila malipo kwa mujibu wa masharti ya leseni za
makampuni ya miundombinu ya utangazaji ya ardhini (DTT) na Satellite (DTH).
Kuhusu muonekano
na wa TBC1 maeneo yote nchini, Naibu Waziri Wambura amesema kuwa Serikali
kupitia Bunge la Bajeti ya mwaka 2017/2018 imetenga jumla ya Sh. Bilioni 3
ambazo ni fedha za miradi ili kuboresha muonekano wa matangazo ya TBC1 nchi
nzima.
|
Friday, September 08, 2017
Vituo 32 Vya Televisheni Nchini Tanzania vyapewa Leseni na TCRA.
Tags
# HABARI
Sambaza Hii
Chief Editor | Mhariri
HABARI
Labels:
HABARI
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
Kuhusu Mwandishi
Journalist / Chief Editor / Tanzanian Blogger
Simu: 0756830214 / 0620197747 / 0789925630.
No comments:
Post a Comment