Chama cha
Wananchi (CUF) upande wa Maalim Seif
kimetangaza misimamo yake baada ya Spika wa Bunge, Job Ndugai kuwaapisha
wabunge viti maalumu saba walioteuliwa na Baraza Kuu la Uongozi linalomuunga
mkono Mwenyekiti anayetambuliwa na Ofisi ya Msajili wa Vyama vya Siasa, Profesa Ibrahim Lipumba.
Wakati
akitangaza misimamo ya CUF mbele ya Wanahabari, Naibu Mkurugenzi wa Habari na
Mawasiliano wa chama hicho, Mbarala
Maharagande amesema Baraza Kuu la Uongozi la Taifa CUF haliwatambui wabunge
hao walioapishwa Septemba 5,2017.
Mbarala amesema CUF haitokubali kutumiwa
kutengeneza upinzani bandia wa kisiasa wa kuendelea kuisaidia CCM kubaki
madarakani, na kudai kwamba haiko tayari kushirikiana na wabunge hao kwa kuwa
wameteuliwa kwa ajili ya kuisaidia CCM Bungeni.
“Jana tumeshuhudia jinsi wafuasi
wa Lipumba walivyopokelewa na wabunge wa CCM Dodoma na kuandaliwa dhifa ya
kusherehekea ushindi wa hujuma dhidi ya CUF. Hii ni mara ya kwanza kaa
wanaoitwa wabunge wa Upinzani kuingia bungeni kuapishwa na kusindikizwa na
wabunge wa CCM,” amesema.
“Kwa hakika spika amepoteza sifa na
haiba ya kuongoza Bunge ambalo ni mhimili wa dola na ambao ulipaswa kuwa alama
ya uadilifu katika nchi, lilipaswa kuwa chombo muhimu cha watanzania katika
kuisimamia serikali ili wananchi wapate maendeleo, lilipaswa kuwa huru chenye
kujisimamia na kuacha kutumiwa kukandamiza upinzani. Ajitathimini aone kwamba
anahitaji watanzania wamkumbuke kwa jambo lipi baada ya kuondoka katika nafasi
hiyo,” amesema.
Wakizungumza
katika mkutano huo baadhi ya wabunge waliovuliwa ubunge wao, wamezitaka baadhi
ya taasisi za serikali kutoshiriki katika kuhujumu mfumo wa demokrasia.
Akizungumza
kwenye mkutano huo, Riziki Ngwali
amesema anasikitishwa na kitendo cha Bunge kuwaapisha wabunge hao kwa madai
kwamba kimelenga kuugandamiza mfumo wa demokrasia.
“Inasikitisha, nchi ambayo ni ya
kidemokrasia imeweka sheria na taratibu za kusimamia mifumo ya demokrasia,
halafu taasisi zinashiriki kuuharibu mfumo huo. Sikutegemea kama ofisi ya
msajili ingefanya hivyo, ni muendelezo wa njama na hujuma,” amesema na
kuongeza.
“Nilimtahadharisha msajili kwamba
anachokifanya kinahatarisha usalama, CUF ni chama chenye nguvu hasa upande wa
Zanzibar. Hivi vilio vya kila mara haviwezi vikaisha kimya kimya. Kuna mwisho
na kikomo, hujuma haisaidii, mkinya haki watu wataitafuta.”
Kwa upande
wake Savelina Mwijage amesema
“Sisi hatulilii kuvuliwa kwetu ubunge,
tunalilia kuathirika kwa chama chetu. Sisi ni wanadamu hatuwezi kusema lolote
Mungu ataamua na mahakama pia itaamua, Spika anachuki na CUF si vingine,”
amesema.
|
No comments:
Post a Comment