Jeshi la
Polisi jijini Dar es salaam limempiga risasi na kumuua muhusika wa matukio ya
mauaji mbali mbali yaliyotokea mkoani Pwani yakiwemo mauaji ya watu Kibiti,
pamoja na wizi katika baadhi ya benki hapa nchini.
Akitoa
taarifa hiyo Kamanda wa Polisi Kanda maalum jijini Dar es salaam Lazaro
Mambosasa, amesema tukio hilo limetokea usiku wa kuamkia leo September 13,2017 katika eneo la
Kivule Chanika, ambapo polisi ilimjeruhi Annae Rashidi Kapela maarufu kwa jina
la Abuu Mariam alipokuwa akijaribu kukimbia, na kufariki dunia akiwa njiani
wakimpeleka hospitali.
"Askari
walipojaribu kumsimamisha aligeuka na kuanza kukimbia, askari walifyatua risasi
na kumpiga kwenye goti, alipokamatwa jambazi huyo alitaja mlolongo wa matukio
yaliyowahi kuyatekeleza, jambazi huyo amekiri kushiriki kwenye tukio la askari
walioawa pale Mbande CRDB, uvamizi wa NMB Mkuranga, Access bank Mbagala, kule
Kibiti ambapo askari 8 waliuawa na silaha
kuchukuliwa", amesema Kamanda Mambosasa.
Kamanda
Mambosasa aliendelea kusema kwamba baada ya jambazi huyo kukamatwa alihojiwa na
kutaja baadhi ya wahalifu anaosaidiana nao kwenye uhalifu, na baada ya kumaliza
kumuhoji alichukuliwa kuwahishwa muhimbili na kufariki dunia akiwa njiani.
|
No comments:
Post a Comment