Job Ndugai -"Hivi nyie watu gani, haya ndio malipo kwa Spika?" - Mwana Wa Makonda

Muhtasari

X-BET


Post Top Ad

Thursday, September 14, 2017

Job Ndugai -"Hivi nyie watu gani, haya ndio malipo kwa Spika?"

Spika wa Bunge wa Tanzania, Job Ndugai.

SPIKA wa Bunge, Job Ndugai amesema anamsamehe Mbunge wa Arusha Mjini (Chadema), Godbless Lema kwa maneno aliyosema kwenye mitandao ya kijamii kwa kuwa hajui atendalo.

Spika Ndugai amesema amesononeshwa na maneno yanayosemwa kuhusu Mbunge wa Singida Mashariki (Chadema), Tundu Lissu kupigwa risasi.

Akizungumza baada ya kutambulisha wageni bungeni leo September 14,2017 Alhamisi, Spika Ndugai amesema wabunge wenyewe ndio waliamua suala la matukio ya watu kushambuliwa kwa risasi liende wa Kamati ya Mambo ya Nje, Ulinzi na Usalama.

Spika amesema Lema anamtuhumu kwa kumpeleka Mbunge wa Ubungo, Saed Kubenea mbele ya Kamati ya Haki, Maadili na Madaraka ya Bunge lakini wao ndio waliamua suala la watu kushambuliwa kwa risasi lijadiliwe na kamati ya ulinzi.

Anasema maneno barabarani ayaseme huko kwa wabunge wenzake,” amesema Spika.

Full video tayari nimekuwekea hapa chini….

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad