Bunge la Tanzania kuanza Leo September 5, Yatakayojiri ni Haya Hapa. - Mwana Wa Makonda

Muhtasari

X-BET


Post Top Ad

Tuesday, September 05, 2017

Bunge la Tanzania kuanza Leo September 5, Yatakayojiri ni Haya Hapa.

Leo September 5, 2017  ni tarehe maalumu ya kuanza kwa Mkutano wa Nane wa Bunge la 11.

Taarifa kutoka Ofisi ya Bunge Dodoma hapo Jana September 4, 2017 ni kwamba ratiba rasmi ya mambo yote makubwa yatakayofanyika kwa kipindi chote wakati Bunge likiendelea.

Taarifa imesema…

Mkutano wa Nane wa Bunge unatarajiwa kuanza kesho Jumanne tarehe 5 Septemba, 2017 na kumalizika tarehe 15 Septemba 2017 Mjini Dodoma. Shughuli zilizopangwa kufanyika katika Mkutano huo ni kama ifuatavyo:-
  1. KIAPO CHA UAMINIFU
Kutakuwa na Kiapo cha Uaminifu kwa Waheshimiwa Wabunge saba wa Chama cha Wananchi (CUF) walioteuliwa na Tume ya Taifa ya Uchaguzi hivi karibuni.  Wabunge hao wapya watakaoapishwa ni:-
  1. Mhe. Alfredina Apolinary Kahigi
  2. Mhe. Kiaza Hussein Mayeye
  3. Mhe. Nuru Awadhi Bafadhili
  4. Mhe. Rukia Ahmed Kassim
  5. Mhe. Shamsia Aziz Mtamba
  6. Mhe. Sonia Jumaa Magogo
  7. Mhe. Zainab Mndolwa Amir
  1. MISWADA YA SERIKALI
Katika Mkutano huu wa Nane wa Bunge jumla ya Miswada mitatu inatarajiwa  kusomwa kwa hatua zake zote.  Miswada hiyo ni :-
  1. Muswada wa Sheria ya Marekebisho ya Sheria Mbalimbali Na. 3 wa Mwaka 2017 (The Written Laws (Miscellaneous Amendments) (No. 3) Bill, 2017) 
  2. Muswada wa Sheria ya Reli wa Mwaka 2017 (The Railways Bill, 2017)
  3. Muswada wa Sheria ya Madaktari, Madaktari wa Meno na Wataalam wa Afya Shirikishi wa Mwaka 2016 (The Medical, Dental and Allied Health Professionals Bill, 2016)
Aidha, Katika Mkutano huu wa Bunge Maazimio matano yanatarajiwa kuridhiwa. Maazimio hayo ni:-
  1. Azimio la Bunge la Kuridhia Itifaki ya Jumuiya ya Afrika Mashariki ya Afya  ya Mimea, Usalama wa Wanyama na Chakula (The East African Community Protocol on Sanitary and Phytonisanitary (SPS) Measures).
  2. Azimio la Bunge la Kuridhia Itifaki ya Amani na Usalama wa Jumuiya ya Afrika Mashariki (East African Community Protocol on Peace and Security.
  3. Azimio la Bunge la Kuridhia Mkataba ya kuanzisha Kamisheni ya Pamoja kati ya Tanzania na Malawi kuendeleza Bonde la Mto Songwe (Convection of Establishment of Joint Songwe River Basin Commission between Tanzania and Malawi).
  4. Azimio la Bunge la Kuridhia Mkataba (Intergovernmental Agreement – IGA) baina ya Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Serikali ya Jamhuri ya Uganda kuhusu Mradi wa Ujenzi wa bomba la kusafirisha mafuta ghafi la Afrika Mashariki. (East Africa Crude Oil Pipeline – EACOP) kutoka Hoima (Uganda) hadi Tanga (Tanzania).
  5. Azimio la Bunge la Kuridhia Itifaki ya Nyongeza ya Tisa ya Mwaka 2016 ya Katiba ya Umoja wa Posta Duniani.
  1. TAARIFA YA KAMATI 
Bunge pia linatarajia kupokea Taarifa ya Kamati ya Kudumu ya Sheria Ndogo kuhusu uchambuzi wa Sheria Ndogo.
  1. MASWALI
Katika Mkutano huu jumla ya maswali ya kawaida 125 yanatarajiwa kuulizwa na kujibiwa Bungeni. Aidha, kwa mujibu wa Kanuni ya 38 (1) ya Kanuni za Kudumu za Bunge wastani wa maswali 16 ya papo kwa papo kwa Mheshimiwa Waziri Mkuu yataulizwa na kujibiwa pia siku za Alhamisi.
  1. TAARIFA ZA KAMATI MAALUM
Katika Mkutano wa Saba wa Bunge la Kumi na Moja Mheshimiwa Spika aliunda Kamati Maalum mbili (2) kwa ajili ya kuchunguza biashara ya Madini aina ya Tanzanite na Almasi

Kamati hizo zilizopewa siku 30 zimekamilisha kazi hiyo na zitawasilisha taarifa zao keshokutwa tarehe 6 Septemba 2017 katika hafla fupi itakayofanyika katika viwanja vya Bunge na kuhudhuriwa na viongozi wa Kitaifa. Katika tukio hilo, Mhe. Spika atapokea taarifa hizo na kuzikabidhi kwa Mhe. Waziri Mkuu. 

Matangazo ya hafla hiyo yatarushwa moja kwa moja katika Channel ya Bunge.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad